“Ruge Alinisaidia Nilikuwa Mwizi Akanirudisha Kwenye Mstari”- Msami

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Dansa maarufu Tanzania Msami Baby amefunguka na kuweka wazi Jinsi Marehemu Ruge Mutahaba alivyomsaidia na kumtoa kwenye maisha ya wizi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Msami alisema kipindi hicho alikuwa akiishi maisha ya kihuni Temeke ambapo alikuwa mwizi wa kutupwa na tena wa kuvunja nyumba za watu, kuiba mali na kwenda kuuza lakini anamshukuru sana Ruge ndiyo ameweza kuona kipaji chake na kumwambia aachane na hivyo vitu aimbe.

Nitalia siku zote juu ya Ruge, ameniepusha na kifo mimi maana jamaa niliyekuwa naiba naye majumbani kwa watu amesh-auawa. Baada ya Ruge kuniona na kunichukua nilisafiri kwenda Afrika Kusini na niliporudi nilikuta yule rafiki yangu kauawa kwa sababu ya wizI”.

Lakini pia Msami ameweka wazi kuwa moja ya mafanikio makubwa aliyokuwa nayo ni Ruge kumuamini kuwa msanii na kiongozi wa madansa na pia kumfanikishia kununua gari aina ya Toyota IST (nyeusi) ambayo imekuwa ikim-saidia katika kazi zake za kimuziki.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.