Sababu Kwanini Nywele Zako Hazikui

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakikata tamaa katika ukuaji wa nywele, wengine ukimbilia kuweka dawa kwa haraka lakini kwa kawaida nywele zenye dawa huwa zinakuwa ila itafika sehemu zitaanza tena kukatika.leo nadhani hii itakuwa inawalenga sana  wale wenye nywel ambazo hazina dawa yaani natural hair.unaweza kuona nywele zako hazikui kabisa kumbe sababu ni hizi hapa.

1.Kunywea

download latest music    

kwa watu wenye nywel natural kuna muda utaona ywele zako wala hazishtuki kurefuka , la hasha wala usikate tamaa ,aina hii ya nywele huwa na tabia ya kunywea na kurudi chini hivyo sio kwamba ni fupi  lakini zinakuwa zimerundikana kwa ndani.

2.Tabia mbovu ya utunzaji wa nywele.

Unaweza kuhisi kama unatunza nywel zako vizuri kumbe ndio kwanza unaziharibu kabisa, wengi wamezoea kutumia moto katika kuzi-style nywele zao,kuweka rangi kwenye nywele au kusuka na kuweka style zinazovua sana nywele na kufanya nywek zikatike.

3.Nywele kuwa kavu sana na kukosa unyevunyevu

ni lazima kujua aina ya nywele zako ili kujua jinsi ya kuzihudumia, kwa kawaida nwele kavu huwa ziankatika tena muda mwingine huweza kukatika kwa speed ileile inayokuwa nayo kwaio kile kinachoingia ndio kinachotoka .hapo tunakuwa unalalamika tu kuwa nywele zako zimedumaa.

4.Zingatia muda wa kukata ncha.

Kuna muda nywele zitataka kupunguzwa ncha ili ziendelee kukua, inakuwa kama mti unaotaka kupunguzwa matawi.Ukataji wa ncha utoa nywele za mbele ambazo mara nyingi zinakuwa zimeharibika na usababisha zile za nyuma zisikuwe kwa wepesi.

5.Jua mzunguko wako wa nywele kukua

Sio kila nywele ukua haraka kama vile unavyofikiri, kuna muda kulingana na mzunguko wako wa nywele.Kuna watu wanamzunguko mrefu na wengine wanamzunguko mkubwa wa nywele kukua, hii ni kulingana na genetics ya mtu.Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa kuna mzunguko wa ukuaji wa nywel wa miaka 2 hadi 6 na nywele uanza mzunguko tena.

6.Uchaguzi mbaya wa vifaa vya kutunzia nywele

Jaribu kutumia vifaa bora katika kutunza nywele zako, usilazimishe kutumia kitana wakati ywele zako i za kuchana na chanuo.Na hata kama ni chanuo basi tumia lenye meno mapana.Vile vile jaribu kutumia mafuta mazuri yanayoendana na nywele zako.Ukiona unashindwa kutambua basi jaribu kuonana na wataalamu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.