Shamsa Ford apasuliwa uso baada ya kupigwa ngumi

Image: Shamsa Ford

Shamsa Ford ‘Chausiku’, amepata jeraha usoni baada ya mwanaume ambaye hajulikani alimpiga ngumi huku akimuacha kama amepasuka na kuvuja damu. Kupitia Instagram Shamsa aliposti picha na kuonyesha mashabiki wake alivyofanywa na mtu huyo.

Jeraha lake limewaacha wengi wakisema kuwa litabaki maisha. Shamsa naye aliandika ujumbe kwa mashabiki zake kuwa alipigwa akiwa anaamua ugomvi. Inasemekana kuwa jamaa aliyempasua uso alikuwa akimtongoza mfanyikazi wa Shamsa kwa nguvu na ndipo muigizaji huyu aliingilia kumsaidia msichana wa wenyewe.

download latest music    
Shamsa Ford
Shamsa Ford

Hata hivyo inaonekana jamaa huyo alikuwa amejaa hasira baada msichana huyo kumkataa na baada ya Shamsa kuingilia, akamtolea hasira kwa kumpiga ngumi ya uso.

Ingawa Shamsa alikuwa akilalamika maumivu makali kichwani, hivi sasa anaendelea vizuri.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua