Tin White Awaponda JB na Wema Sepetu.

Mchekeshaji maarufu bongo Tin White ameibuka na kumchana wema sepetu pamoja na JB  kwamba sio wasaniiwa ukweli ila washukuru mungu kwa kufika hapo walipo sasa kutokana mitandao ya kijamii mbayo imekuwa ikiwakuzia majina yao.

Tin White ameongea hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha eNews,baada ya kuwepo kwa wimbi la wasaini wengi kwa sasa ambao wamekuwa wakiingia katika sanaa bila kupitia vyuo vinavyohusiana na sanaa hivyo wamekuwa wakiharibu tasnia hii ya sanaa.

Unajua kuna kipaji yaani hiyo ni reality kabisa lakini pia kuna muongezo wakina kanumba walikuwa wanafanya kwa  vipaji  vyao vyenyewe tu lakini hawa wakina wema sepetu  walikuja tu kujaribu hao sasa ndo wa kuongezea .

mimi naongea ukweli kabisa  kutokana na mitandao ndo maana wakina Wema Sepetu wameweza kuitika  lakini hana reality yoyote ile.Hata huyo JB hakwa na historia ya kuwa msanii  alikuwa anauza mahindi ila yeye alilazimishwa na Single Mtambalike ili awe msanii siongei kwa ubaya ila naongea jambo la ukweli kabisa.

 

 

Mwanakheri na Niva Ndani ya Bifu Zito.

Wasanii wa bongo movies Niva pamoja na Mwanakheri wanasemekana wapo kwenye bifu zito ambalo limesababishwa na msanii mwenzao Riyama Ally.Baada ya kuchunguza kwa muda mrefu ilikuja kubainika kuwa wasanii hao wawili wapo katika bifu zito kwa  zaidi ya miaka miwili.

Sababu kubwa ya wawili  hao kuwa na bifu ni baada ya niva kumkataza mwanakheri kuwa anamtukana Riyama Ally kwa sababu yeye ndio aliemtambulisha katika tasnia ya maigizo.

Kampuni ya GPL  waliamua kumtafuta Niva ili aweze kuthibitisha swala hilo ambapo alikiri kuwa ni kweli yeye na Mwanakheri hawapo katika mahusiano mazuri na hii yote ilitokana na yeye kumkanya msanii huyo kuacha kumtukana mwenzake kwa kuwa ndie aliemtambulisha katika game.

Hata hivyo baada ya kumtafuta mwanakheri kumuuliza swala hilo alikana na kusema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu yeye kumtukana Riyama na hata huyo Niva hawaingei kwa sababu sio rafiki yake.

Sijawahi kumtukana riyamma,na huyo niva hajawahi kunirekebisha kwa kitu chochote  ila sipo nae kribu kwa sababu sio rafiki yangu.

 

Bongo Movies Wanaounda Kundi La Uzalendo Wamkataa Steve Nyerere

Wasanii wa bongo movies ambao wanaunda kiundi la Uzalendo Kwanza wameamua kujiweka pembeni  na kuacha kukitumikia kikundi hicho na kweka pembeni kabisa   harakati hizo kwa madai kuwa hawamuelewi kabisa mwenyekiti wao wa kikundi hicho Bwana Steve Nyerere ambae amekuwa akijinufaisha mwenyewe na kuacha dhana ya uzalendo kwanza.

Wasanii hao wakiongozwa na viongozi wengine kama Davina,Dude na Thea wamesema kuwa hawamuelewi mwenyekiti wao kwa sababu kila kukicha anafanya vitu kwa kutumia kundi hilo kujinufaisha yeye mwenyewe bila kujali kuwa kundi limeundwa na watu wengi na lina malengo mengi.

Viongozi hao walisema kuwa wameamua kujiweka pembeni ili kuepusha ugomvi usiokuwa na tija kwa sababu kipindi wanaanza hawakuwa na lengo baya zaidi ya kuleta uzalendo, na wanasema kuwa pamoja na kwamba wameamua kujiengua lakini bado haki zao ziko palepale kwa sababu wao pia ni waanzilishi wa kundi hilo.

Kundi la Uzalendo Kwanza lilianzishwa miaka miwili nyuma kipindi cha kampeni za uchaguzi ikiwa na lengo la kuhamasisha uzalendo kwanza kwa wananchi na kuacha maslahi ya mtu moja moja katika kuchagua viongozi wa nchi.

Steve Nyerere  amekuwa akikumbwa na kashfa nyingi za kisiasa ambapo hivi karibuni alionekana hata kumkosoa kiongozi mmoja wapo mkubwa wa chama kilichopo madarakani baada ya msanii Wema Sepetu kutangaza kurudi CCM, hata hivyo kundi la uzalendo kwanza linaweza kuwa limemkataa mwenyekiti huyo kwa madai ya kile kuwa kipindi Wema anaondoka CCM kwenda CHADEMA  alileta maneno maneno  ya kugombana na wanakikundi hicho na kusema kuwa walikuwa wakifanya kampeni bila kulipwa ambapo wasanii wa kundi hilo walimjia juu ,ambapo aliingia ktika ugomvi na msanii mwenzie Batuli  , lakini kitu cha kushangaza ni kwamba hata baada ya msanii huyo kuamua kurudi bado Steve Nyerere  aliweza kumpokea .

 

Wafahamu Wasanii Wenye Mvuto Zaidi Bongo Movies

Hawa ni wasanii wa kike bongo movies ambao wamekuwa katika rekodi ya wasichana wenye mvuto zaidi.

ELIZABETH LULU MICHAEL

Ameanza kazi ya sanaa akiwa bado na umrri mdogo sana na mpaka sasa anafanya vizuri sana, Amepitia misukosuko mingi ambayo imemfanya kuwa imara zaidi katika maisha yake.Lulu uonekana maridadi na mwenye mvuto kila iitwapo leo.kwa malkia wa bongo movie yeye anaweza kuwa ni namba moja.

YOBNESH YUSUPH(batuli)

ni mwanamama mwenye mtoto mmoja wa kiume, lakini mvuto na urembo wake ambavyo anazidi kuutunza huwezi kuzania kuwa ni mzazi.

IRENE UWOYA

Tangu kuwa miss Tanzania mpaka sasa, irene amekuwa moja ya wasichana wanaongoza kuwa na muonekano mzuri, mwili wake haubadiliki na mavazi yake umfanya kuwa maridadi na mwenye mvuto zaidi.

WEMA SEPETU.

Wema Sepetu, mwanadada anaependwa karibia na Tanzania nzima, ni msanii wa kike anaeongoza kuwa na followers wengi  tanzania. Wema hachuji kwa uzuri na hakuna nguo atakavyovaa ikaacha kumpendeza .

WELU MATILDA SENGO

Malkia wa bongo movie alikuja kwa kasi katika tasnia, pia anafanya vizuri akiwa katika kazi yake.