Wema Afunguka Kudhulumiwa Milioni 64 na Mwanaume Aliyehaidi Kumuoa

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweza wazi kuwa amekuwa akipitia kipindi kigumu tangu alipoachana na aliyekuwa Mpenzi wake Patrick ambaye pia alimdhulumu milioni 64.

Wema Sepetu ameeleza kuwa ameanza upya maisha kutokana na misukosuko aliokutana nayo ya kutapeliwa shilingi milioni 64 na aliyemdanganya anataka kumuoa, Patrick Christopher ‘PCK’.

download latest music    

Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Wema alisema kuwa mwanaume huyo alimtapeli kiasi hicho cha fedha hivyo amejifunza kutokana na makosa na anamuomba Mungu asirudie tena kosa kama hilo lililotokea maana angekuwa ameshafanya vitu vingi vya maana ambavyo vingemsaidia kwenye maisha yake.

Nilipita kwenye kipindi kigumu sana jamani, nimerudi nyuma sana yaani kifupi naanza maisha upya na mpaka sasa siamini kile ambacho kilinitokea yaani kama mtu alinipumbaza sijui kwa nini ila kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ndiyo kosa”.

Wema ameweka wazi kuwa amekuwa hayupo kwenye mahusiano kwa miezi sita sasa na hataki mwanaume kwani yupo bize kujenga maisha yake.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.