Lulu Kuwapa Zawadi Mashabiki Siku ya Valentine.

Mwanadada Elizabeth Lulu  Michael ameamua kukutana na mashabiki zake katika siku ya Valentine yaani siku ya wapendanao ambayo kila mwaka ufanyika February 14.

mwanadada huyo ambae hapo awali aliwahi kusema kwamba kupitia  ukurasa wake kuwa anategemea kugawa nguo zake zote ambazo ziliwahi kuvaliwa nae huko nyuma na kuwataka wale wote waliotamani kupata moja ya nguo zake wafanya ku-comment katika ukurasa wake lakini ameamua kubadili uamuzi huo na kuja na kitu vha tofauti.

Akiita siku hiyo save the valentine, lulu anategemea kufanya  kama mnada wa nguo zake pendwa ili pesa itakayo patikana katika siku hiyo bas itakwenda kusaidia kuwapa wale wote wenye mahitaji mbalimbali katika sehemu mbalimbali.

 

 

“Natamani Kuzaa” Elizabeth Michael ‘Lulu’ afunguka kuhusu kuwa mama

Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni mmoja wa wanawake maarufu Tanzania kwa sababu ya sinema za Kibongo. Hata hivyo wenzake wamekuwa wakizaa na kulingana na mahojiano yake na 4-Tamu pia yeye anatamani mtoto.

Hii ni mara ya kwanza kwa Lulu kusema haya. Katika mahojiano yake Lulu alisema kuwa imefika wakati na yeye anatamani sasa kuzaa.

Aliendelea kusema kuwa umri wake unamruhusu na akipata mwanaume wa kumzalia basi atajaribu kupata mtoto. Akizungumza na 4-Tamu alisema;

Lulu Micheal

“Natamani tu na mimi nipate mtoto sema ndiyo hivyo bado natengeneza mipango ya mimi kuwa mama tena mama bora,”