Nini cha Kufanya ili Kulinda Mahusiano Mapya

Hisia za mapenzi na msisimko huwa mkubwa  kipindi ambacho upo kwenye penzi jipya. Ukiwauliza watu wengi leo ambao wanateswa na mapenzi, wanata­mani siku zirudi nyuma ili warudie kufaidi mapenzi kama ilivyokuwa siku za mwanzomwanzo.

Lakini wachache wanaojua nini cha kufanya unapoanzisha penzi jipya ili hisia na msisimko unaoupata, udumu kwa muda mrefu na uendelee kuyafurahia maisha ya kimapenzi. Mapenzi ni kama nyumba, ukijenga msingi imara, nyumba yako itakuwa imara na ukijenga msingi legelege, usitegemee nyumba yako kuja kudumu baadaye.

Kama upo kwenye mapenzi mapya na unatamani raha na msisimko unaoupata leo udumu, ni vizuri ukazingatia mambo yafuatayo:

MUONYESHE HESHIMA NA SHUKRANI

Wanandoa, wachumba au wapenzi wengi, hulalamika kwamba wenzi wao hawawaheshimu, hawana shukrani na ndiyo maana hawafurahii maisha yao ya kimapenzi. Unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za mapenzi, jenga heshima kwa mwenzi wako bila kujali umri, cheo au hali ya kiuchumi. Hata kama mwenzi wako ana udhaifu fulani, kwa sababu umem­penda na kuamua kuwa naye, jifunze kumheshimu.

Pia jifunze kuwa na shukrani hata kwa yale mambo ma­dogo anayokufanyia. Wen­gi huwa hawaoni umuhimu wa kuwashukuru wenzi wao na matokeo yake wanajenga ufa am­bao baadaye unasa­babisha matatizo makubwa.

 

PATA MUDA WA KUMCHUN­GUZA KWA KINA

K u c ­h u n g u ­zana nina­komaani ­sha hapa, siyo ku­taka ku­jua kabla y a k o alikuwa na nani au amewahi kutoka na nani, wahenga wanasema bata ukimc­hunguza sana huwezi kumla. Kuchungu­zana ninakokuzungumzia hapa, ni vizuri kufuatilia kwa kina ili ujue mwenzi wako anapenda nini, hapendi nini, kitu gani kinamfurahisha na kitu gani kinamtia hasira.

Mchunguze akiwa na hasira anakuwa­je na akiwa na furaha anakuwaje, ana­penda sana kufanya mambo gani (hobi) au anapenda sana zawadi za namna gani. Ukishamjua, ni rahisi sana kuishi naye hata pale anapokasirika au ana­pokerwa na jambo fulani kwani tayari utakuwa unajua kwamba akiwa hivi, ujue amekasirika au akifanya hivi ujue jambo fulani halipendi.

Pia itakusaidia kwenda naye sawa kwa sababu akikasirika, utajua ufanye nini ili afurahi kwa sababu tayari unavi­jua vitu vinavyomfurahisha. Ni makosa makubwa kufanya jambo wakati unajua kabisa mwenzi wako hapendi.

JENGA UTARATIBU WA KUMUOM­BA MSAMAHA UNAPOKOSEA

Wanaume wengi wanaamini kwamba hata wakikosea, hawatakiwi kuomba msamaha kwa sababu kuomba msama­ha ni ishara ya udhaifu, matokeo yake wanaendekeza mfumo dume bila kujua kwamba mapenzi ni demokrasia!

Bila kujali kwamba wewe ni mwa­naume au mwanamke, mkubwa au mdogo, una fedha au huna, inapotokea umeziumiza hisia za mwenzi wako, iwe kwa jambo dogo au kubwa, ni lazima uombe msamaha na kuahidi kutorudia makosa.

Ukishajenga utara­tibu huu, hata kama mwenzi wako hakuwa na kawaida ya kuom­ba msamaha, tara­tibu utambadilisha. Utashangaa na yeye anaomba msamaha na huo unakuwa mfu­mo wa maisha yenu. Kuwa makini kwamba ukiomba msamaha leo, siyo kesho unarudia tena kosa lilelile, ataona unam­fanyia makusudi.

 

Sababu Za Wanaume Kutoka Nje ya Ndoa.

Wanaume wengi wamekuwa na tabia ya kutoka nje ya ndoa ambapo kwa zamani ilikuwa si kitu cha kawaida  na hata walipokuwa wanafanya ilikuwa inafanyika kwa siri sana, lakini  sasa hivi imekuwa ni jambo la kawaida na inawezekana kila mtu akajua na hata mke wake  anapojua kwa mwanaume anaona ni kitu cha kawaida tu.

Inawezekana kuwa mwanaume anafanya makusudi kufanya bila kuwa na sababu ya kufanya hivyo.unaweza usimuelewe mtu anapokwambia sababu za yeye kuchepuka lakini kitu chochote kinapozidi ufanya mtu kuchoka na kutafuta mbadala.

mapenzi.

Inatokea kuwa mwanaume anaona mwanamke wake amtoshelezi kimapenzi kabisa na kila akijitahidi kumrekebisha ni kama vile hamuelewi kabisa.kwenye mapenzi kuna ubunifu na vitu vingi vinavyoitajika ili kumridhisha mwenzi wako hivyo pale mwanaume anapoona kuwa kila siku wewe ni yuleyule ndipo anapotafuta kupya.

kisasi

Mwanaume mwingine sio msemaji kama mwingine, anapohisi kuwa mwanamke aliyenae anamahusiano ya nje anachofanya  yeye ni kulipiza bila kuwa na uchunguzi , na hata kama itakuwa ni uongo kwa mwanamke endapo mwanaume atajaribu nje na kuona utofauti basi ujue mwanaume huyo tayari ameshapotea.

mabishano ya kila siku.

wanaume wengi sio waongeaji kama wanawake, linapotokea jambo dogo ni vigumu mwanamke kulinyamazia tofauti na mwanaume ambae huweza kukaa nalo muda mwingi kwa sabau tu hataki kuongea sana, hivyo inapotokea kuwa kila baba akirudi nyumbani basi lazima kesi zianze ni lazima atatafuta ambapo akienda anakaribishwa na utulivu na mahaba tele.

mapishi.

Hii pia huwa ni sababu kubwa sana wanaume uwafanya kuhama nyumba zao,baba anakuwa anachika kula mapishi yale yake kila siku.Mara nyingine chakula kinakosa radha, muda mwingi jikoni anashinda dada wa kazi, mwanaume anaamua kula hotelini na siku akichoka akaonja mapishi tofauti tu basi shoga baba unampoteza.

kubadilika na kuwa sio kama zamani.

Nadhani kuna muda unafika mwanamke anakuwa namzoea sana mumewe kiasi kwamba kuna vitu alikuwa anafanya mara ya kwanza anabadilika na kuacha kuvifanya tena.Anaweza kuwa sio msafi kama zamani, lugha zake sio nzuri tena, hamjali tena mwanaume wake , hii itamfanya mwanaume kwenda kutafuta mambo hayo sehemu nyingine.

 

 

 

Umuhimu wa Tendo la Ndoa Kiafya (+18)

Wataalamu wanasema kuna umuhimu kubwa kwa mwanadamu kufanya tendo la ndoa kwa ajili ya kuimarisha afya yako,kwanza kabisa inapunguza mafuta mwili lakini pia inasemekana kuwa endapo mtu anafanya tendo la ndoa mara tau kwa wiki ndani ya mwaka mzima ni sawa na kukimbia  maili75,tendo la ndoa uongeza vizalishi 150 katika mwili ambapo kwa nusu saa ni sawa na kukimbia dakika 15.Sio hayo tu umuhimu mkubwa wa tendo la ndoa unakuja katika yafuatayo’

kuongeza mwendo wa damu mwilini.

Tendo la ndoa uongeza kasi ya mtiririko wa damu katika mwili wa mwandamu, hasa katika ubongo na sehemu mbalimbali, lakini pia hii usaidia zaidi usaidia zaidi kasi ya mapigo ya moyo na katika mfumo wa upumuaji.

Msukumo mzuri wa damu mpya yenye oxygen husaidia zaidi katika uunguzaji mzuri wa chakula lakini pia ni vizuri kwa sababu usaidia kutoa uchafu katika mishipa ya damu ambayo ingeweza kumfanya mtu kuumwa mwili.

Kupunguza mafuta mwilini(cholestrol)

Tendo la ndoa uweka uwiano sawa kwa mafuat yenye kileo mwilini yaani kwa ile iliyo mbaya na hata ile iliyo nzuri uziweka sawa ili mwili ufanye kazi kwa uwiano sawa.

Kupunguza maumivu ya mwili

wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo hii uchangia kwa kiasi kikubw akutengeneza kwa  endorphini ambayo husaidia kupunguza maumivu ya mwili  kama vile kuvimba sehemu mbalimbali za viungo(arthitis) , shingo (whiplash) na maumivu ya kichwa.

Kupunguza mfadhahiko ya moyo na kuondoa msongo wa mawazo.

Inaaminika kwamba mara nyingi watu wanaoshiriki tendo la ndoa mara kwa mara ni watu wenye tabasamua muda wote,hii ni kwa sababu mara mtu anapofanya tendo la ndoa na kupata muda wa kupumzik ahujikuta akijisikia vizuri na mwenye nguvu muda wote.wapo wachache waliowahi kuthibitisha kuwa wanapata usingizi mmno wanapomaliza kufanya tendo la ndoa na kulala,lakini pia wengi wamekuwa wakikiri kuwa siku zao huwa njema wanapopata muda wa kufanya tendo la ndoa asubui kabla ya kuingia katika kazi na majukumu mbalimbali.

Kuishi Muda mrefu huku ukionekana kijana.

Wakati wa kufanya mapenzi homoni iitwayo DHEA uzalishwa mwilini na kusababisha msisimuko katika mwili, homoni hii uwa na kzi kubwa ya kurekebisha mwili,kuongeza ufahamu,kumiarisha mifupa na kutengeneza afya ya moyo.

kuondoa baridi na mafua.

Elimu inaonyesha kuwa wanaofanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa  chembe chembe hai za mwili kwa 30% , chembe hizo ulinda mwili kutopatwa na magonjwa.