Harmorapa atoa ushauri huu kwa Rais Magufuli

Baada ya kumalizana na Wema Sepetu, Harmorapa amejipandisha cheo na sasa lengo lake ni Rais.

Harmorapa ako na ushauri kwa Rais Magufuli ambao angetaka atilie maanani.

Hivo ndivyo alivyomweleza:

“Rais Magufuli unajua yeye ndiye mwenye nchi sasa, hivyo mimi namuomba aboreshe zaidi suala la miundombinu natambua amefanya mambo mengi na makubwa kwenye sekta hiyo ila aboreshe zaidi, lakini pia namuomba Rais Magufuli aendelee kuwafinya wale wajanja wajanja kama ambavyo anafanya saizi na kingine atuangalie na sisi wasanii na kazi zetu”