Ndoa ya Sasha Yavunjika ,Ni Baada ya Kukatazwa Kutumia Mitandao

Ile ndoa ya msanii Sasha Khassim iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na msanii huyo imevunjika na haitafanyika tena kama awali ilivyokuwa imetangazwa na mwanadada huyo.sasha amesema kuwa kama kuna watu walikuwa wakisubiria ndoa hiyo basi wajue kuwa haipo tena na hata mahali haitarudishwa.

Akizungumza na GPL, Sasha amesema kuwa mwanaume huyo alijulikana kwa jina la Boniphace, wameshindwa kumudu nae katika  mapenzi na ameona kuwa hawzi kuwa nae kwa sababu ya wivu wake.sasha anasema kuwa mwanaume huyo amekuwa akikasirika sana kila anapokuta ameposti picha katika mitandao ya kijamii na kufikia hatua ya kumwambia kuwa aachane na mitandao ya kijamii kitu amcacho yeye hawezi kwa sababu hata yeye alimpata kupitia mitandao ya kijamii.

sasha anasema kuwa hayuko tayari kuacha kuweka picha katika mitandao ya kijamii hivyo ni bora aachane na mwanaume huyo.suala la ndoa halipo tena,yeye alinipa katika mitandao ya kijamii lakini cha ajabu ananikataza kabisa kutumia mitandoa ya kijamii.nimeona sitaweza kujinyima uhuru  wa maisha yangu kiasi hiki, hivyo uchumba umevunjika na mpango wa kurudisha mahali haupo kabisa.  -Alifunguka Sasha.

Mwanadada huyo amekuwa akijitapa kwa muda mrefu kuwa  ataolewa na mwanaume kutoa nje ya nchi na atakuwa akifanyakazi zake nchini na kurudi nje kwa mumewe lakini ndoto hizo zimevunjika baada ya kushindwa kuweka mambo sawa.

Sasha Aelezea Alivyoteswa Na Kifo Cha Ndikumana.

Mmoja wa wauza nyago nchin katika video za wasanii mbalimbali  anaejulikana kama Sasha Kassim amefunguka na kusema kuwa alipokea kwa uzuni sana habari za kifo cha  mchezaji wa mpira  Hamad Ndikumana kwa sababu katika watu  aliokuwa akiwapenda tangu zamani ilikuwa ni kuwaona irene uwoya akiwa na mwanasoka huyo.

Sasha anasema kuwa alikuwa akivutiwa sana anaposoma taarifa za wawili hao  na  kusema kuwa kwake ilikuwa ni couple bora sana kuliko couple zozote Tanzania na ndio maana aliumia sana kusikia Ndikumana amefariki Dunia.

mwanadada huyo anaendelea kusema kuwa kwa muda wote wa msiba huo hakuwa na mood ya kufanya kitu chochote kile zaidi ya kukaa ndani kwa huzuni aliyokuwa nayo baada ya kupata taarifa hizo.

Katika couple ambayo nilikuwa nikiipenda sana ni kati ya Ndikumana na Irene Uwoya tangu kipindi nasoma.Nilikuwa napenda kuwasoma na kuwafatilia katika  magazeti sana , na kwakweli kifo cha Ndikumana kimeniumiza sana sana. Alifunguka mwanadada huyo ambae alionekana kuwa na huzuni.

Marehemu Ndikumna enzi za uhai wake akiwa na mtoto wake aliyezaa na Uwoya

Ndikumana alifariki Dunia wiki chache zilizopita  mwezi huu na kuzikwa huko kwao Rwanda ambapo alifariki kwa matatizo ya ugonjwa wa moyo kwa ghafla .Hata hivyo kifo hicho kilizua gumzo na kusemekana kuwa ugonjwa wa mwanasoka huyo ulisababishwa na mawazo ya muda mrefu kutokana n akumuwaza mkewe Urene uwoya alieolewa hivi juzi juzi na msanii wa bongo fleva.

Irene alipata bahati ya kutembelea kaburi la mwanasoka huyo akiambatana na familia yake yaani mama yake na mtoto wao wa kiume mpaka rwanda ambapo alipokelewa vizuri na familia ya Ndikumana tofauti na vile watu walivyofikiria kuwa angeweza kukataliwa na ndugu wa marehemu.Ndugu  wa Ddikumana akiwepo baba yake  walimpa baraka zote Irene Uwoya na kumuombea mazuri.