Uvaaji wa Hereni Kama Pambo

Heleni ni pambo kama yalivyo mapambo mengine lakini limekuwa likiongeza mvuto sana wa mtu hasa usoni na kuonekana mngavu kulingana na uchaguzi wa heleni.

Kuna heleni za ainambalimbali zimetengeneza kwa vitu tofauti tofauti kama dhahabu, shaba, kopa , lakini pia zito zile za asili ambazo na zenyewe sasa hivi zimekuwa zikipamba moto katika uvaaji sana.

download latest music    

Hereni za vifuu vya nasi na pia shanga kwa sasa zinapenda sana na wanawake wengi ingawa hapo awali zilikuwa zikivaliwa sana katika shughuli za kiasili hasa katika jamii ya umasaini kwa upande wa shanga.

Katika uvaaji wa hereni ni lazima uangalie aina ya nguo uliyovaa kwanza lakini pia na rangi ya nguo na eneo unalokwenda pia.wengine uangalia hata nywele walizonazo kichwani ili ku-match na kupendeza.

Kwa mfano uvaaji wa hereni kwa kwenda kanisani ni tofauti na kwenda harusini, au mtoko wa kawaida tu ambao unakuwa labda na mizunguko mingi.wapo wanaopenda kuvaa heleni mara zote na mahali pote , watu wa aina hii unatakiwa uchague heleni ambazo hazitakuwa zinakusumbua sana yaani zisiwe ndefu.

 

Wapo wanaopenda kuvaa hereni  matundu mengi katika sikio moja, basi hii pia inahitaji ubunifu katika kuzipanha ya kwanza mpaka idadi unayotaka ila tu angalia usije ukaonekana kituko.

Wapo pia wanaume wanaopenda kuvaa hereni , hawa wanashauriwa pia kuvaa hereni kulingana na jisnia yao, na mara nyingi wanaume upaswa kuvaa hereni ndogo na zisizoonekana sana.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.