Alichosema Young Killer baada ya Diamond kuamua kutoa wimbo naye

Nyota ya Young Killer sasa inakaribia kung’aa vizuri, rapa huyo ataingia studio na Diamond Platnumz kurecord ngoma mpya itakayompa umaarufu nje ya Tanzania.

Msanii yeyote ambaye amewahi kufanya kazi na Diamond anajua vizuri thamani ya kumshirisha Simba kwa kolabo yoyote ile.

download latest music    
Young Killer

Young Killer sasa amefunguka kuhusu kazi atakayofanya na hit maker huyo wa ‘Marry You’. Rapa huyo alisema mama yake alifurahishwa sana na kitecho cha Diamond kuamua kumshirikisha kwenye moja kati ya nyimbo zake zinazokuja.

Akiongea na Bongo5 hapo jana Mai tarehe nne, Young Killer alimmwagia sifa Diamond na kumtaja kama msanii anayekuza vipaji Tanzania.

“Hiki kitendo kimenifanya nimuone Diamond Platnumz ni binadamu na ni mtu ambaye anastahili kuwepo sehemu ambayo yupo. Ni tukio ambalo limenitia faraja kiukweli hata mama yangu alivyosikia alifurahia sana na kumshukuru kwa kitendo ambacho amenifanyia,” alisema Young Killer.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere