Collabo ya kimataifa: Harmorapa aingia studio na Kriticos – staa kutoka Ubelgiji

Nyota ya Harmorapa yazidi kung’aa hata kama watu wengi bado wanamdharau. Msanii huyo alitupiwa chupa wiki chache zilizopita alipokuwa akitumbuiza mashabiki.

Hivi juzi tu Jackline Wolper alidai kuwa Harmorapa anaudhi sana. Mrembo huyo alisema kuwa hapendi vitendo za rapper huyo.

download latest music    

Soma pia: Jacqueline Wolper: Harmorapa anaudhi sana

Harmorapa hata hivyo hana muda na wanaomchukia, staa huyo wa Bongofleva anafanya collabo na mwanamuziki Kriticos kutoka Ubelgiji.

Msanii huyo mwenye asili ya Tanzania na Zambia, amefika nchini kufanya kazi na Harmorapa ambapo leo April 7, 2017 walipata nafasi ya kuzungumza na AyoTV Entertainment

Harmorapa na Kriticos

Harmorapa amewataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea ngoma hiyo itakayotengenezwa na mtayarishaji wa muziki P-Funk Majani.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere