“Diamond and Ali Kiba wanazuia mziki wa Tanzania kuenda mbali” Professor Jay asema

Ingawa Professor Jay ni rafiki yake Diamond na hata washawai toa kolabo “Kipi Sijasikia”, msanii huyo anasema beef kati ya Diamond and Ali Kiba inazuia mziki ya Tanzania kuenda mbali.

Professor Jay na Diamond

Professor Jay anaamini mziki wa Bongo ingeenda kwenye level nyingine iwapo mashabiki wa Diamond na Ali Kiba wangekuwa pamoja ili kuipigania Tanzania.

download latest music    

Jay alisema haya alipokua akiongea kwenye Ayo TV.

‘Kitu kikubwa ukiongelea beef iliyopo kwenye bongo fleva ni hii ya Diamond na Ali Kiba nadhani mashabiki wa Diamond na Ali Kiba wangekuwa pamoja ili kuipigania Tanzania kwenda kwenye level nyingine nadhani muziki wetu ungeenda  mbali, kwa hiyo moja kati vitu ningependa kushuhudia siku moja Diamond na Alikiba wakiwa pamoja ikifanikiwa tu hiyo naamini muziki wa Bongo unakuwa level nyingine” Professor Jay alisema.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere