“Diamond anapelekwa kwa shimo na watu watatu” Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers aonya

Eric Shigongo, mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, amekiri kuwa Diamond ni mfano mwema wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi Tanzania na ata duniani kote.

Shigogo amesema hit maker huyo ameweza kuvuka vizingiti vyote maishani na kuwa msanii wa kutajika nchini Tanzania na ata barani.

download latest music    

Lakini Shigogo ameonya kuwa Diamond anaelekea shimoni. Mmiliki huyo wa Global Publishers aliandika barua yenye ujumbe kwa Diamond kupitia mtandao wa Instagram;

“Nampenda Diamond sana, tena sana (sina uhakika kama analifahamu hili). I am too proud of him! Ni fighter (mpiganaji), from Tandale to Beverly Hills with Neyo kwenye Video ya Wimbo wa Mary You ambao nimemaliza kuuangalia kwenye YouTube hakika si kitu kidogo.

“ Nafahamu kwa sababu nimeanzia chini sana kimaisha. Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania. Bila elimu ya kubwa, bila connection, bila fedha ameweza kuvuka vizingiti vyote hadi hapo alipo. Hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. BRAVO! LAKINI ninayo machache ya kusema na ninaomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi, kaka na Mtanzania mwenzake. Huko ANAKOELEKEA DIAMOND KUNA SHIMO, ASIPORUKA ATATUMBUKIA NA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE. Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu, nao ni NASEEB ABDUL, BABU TALE NA SALAAM. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti.”

Eric Shigongo na Diamond

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere