Diamond araruliwa kwa kuandika Kiingereza kibovu kwenye Instagram

Diamond hana pakuficha uso wake baada ya kutumia Kiingereza kibovu kutangaza kuwa amezindua manukato yake ambayo ataanza kuuza hivi karibuni.

Staa huyo wa Bongo flava aliongelea kuhusu ujio wa Chibu Perfume akitumia Kiingera ambacho hakikuzingatia sheria ya msamiati ya lugha hio.

download latest music    

“I feel incompleted when am on any outfit, without wearing @chibuperfume !….. @chibuperfume by Diamondplatnumz comming out this week!” Diamond aliandika.

Maneno ‘incompleted’ na ‘comming’ ambazo Diamond alitumia kwa sentensi yake ilikua imeandikwa vibaya – hazina maana yoyote katika Kiingereza.

Wanaofahamu Kiingereza vizuri walimrarua Diamond kwenye comments zao. Wengi walimwambia atumie tu Kiswahili badala ya kujiaibisha na Kiingereza kibovu.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere