‘DNA ifanyike kuweka wazi,Nillan ni mtoto wa nani?’ Zari Hassan na Diamond Platnumz au Ivan!

Maisha ya Diamond Platnumz na baby mama wake Zari Hassan,yamekua kama vile bongo movie,kila wakati lazima usikie mastori kuhusu hili na lile,ni kero wanasema.

Babake Diamond Platnumz,mzee Abdul Juma amefunguka kuhusu tuhuma kuwa, mtoto Nillan sio mwanawe,na Zari Hassan.

download latest music    

Stori zilitamba kwenye mitandao eti Nillan amefanana sana na Ivan,mpenzi wa zamani wa Zari ambaye pia ni baba ya watoto wake.

Mzee Abdul anasema,’ili kuwazima wale wenye dhana potofu kwamba mtoto si wa Diamond ni lazima vipimo vya DNA vifanyike.’

Anaendelea kusema,’Mimi kama mzazi namshauri Diamond akapime DNA ili apate uhakika zaidi japokuwa tunaamini hao wajukuu wetu ni watoto wake lakini kwa kuwa maneno yamekuwa mengi kila kukicha ni lazima afanye hivyo, naamini na maneno ya watu kumsimanga yataisha.’

 

Cha kuumiza zaidi amekiri,’Katika maisha ya kawaida kwa mwanaume ni aibu kulea watoto ambao unajua kabisa si wako lakini unasema ni wako. Mpaka Diamond anaamini ni watoto wake na sisi ndugu tunaamini hivyo, kwa nini wengine wasikubaliane na ukweli huo.’

Habari hii imezua gumzo kwenye mitandao ya jamii,baada ya kutokea kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti.

 

About this writer:

Irari Ngugi

Lover of life, lover of big boobs and certified celebrity squasher. Catch me if you can on facebook as Irari Ngugi