Hasara 5 za Mitandao ya Kijamii

Mitandao ya Kijamii imekua kwa kasi ya ajabu sana kuanzia mwaka 2006 mpaka leo tofauti ni kubwa sana. Kuanzia Facebook, twitter, Instagram mpaka Youtube zimekuwa kwa kasi ya ajabu na kukusanya mamilioni ya watumiaji.

Kila kitu kina faida na hasara pia naweza kusema kuwa mitandao ya kijamii ina athari kubwa sana katika jamii, pia imeweza kurahisisha mambo mengi sana katika jamii yetu inategemea na mtumiaji anayetumia.

download latest music    

Zifuatazo ni baadhi ya Hasara za kutumia mitandao ya kijamii:

1. Kuvunjika kwa Maadili yetu

Mitandao ya kijamii kama yalivyo maendeleo yoyote yameletwa na wazungu hivyo hasa kwa nchi zetu za Afrika zimeonja utandawazi wa hali ya juu ila sisi waafrika tuna mila na desturi zetu ambazo ziko tofauti na wazungu baadhi ya vitu vilivyoharibu maadili yetu ni ukiingia kwenye mtandao wowote wa kijamii utakutana na matusi yaliyopitiliza yaani lugha ambayo watu wanatumia utakimbia. Pia vijana kufuata wanayofanya wazungu na kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, kupiga picha za uchi n.k.

2. Majanga Kama Vifo

Kupitia mitandao ya kijamii hasa facebook au Instagram watu wanakutana wanachat lakini hawajuani wanahis mtu unayeongea naye ni mtu mzuri kuja kuonana wengi wanaishia kuuliwa au kubakwa. Kuna stori niliisikia hapa hapa Tanzania msichana kakutana na mvulana facebook wakapendana ingawa hawajawahi kuonana siku wakasema wakutane Magomeni, yule msichana hakuonekana tena wamekuja kukuta maiti yake Bagamoyo.

3. Wizi na Utapeli

Kwa bahati mbaya mitandao ya kijamii inatumika vibaya sana tofauti na lengo au sababu zilizowekwa kuna watu wanatumia mitandao ya kijamii kuibia wengine yaani utapeli kwa kuuza vitu feki  na kadhalika.

4. Uzembe

Mitandao ya kijamii imesababisha uzembe na kujiendekeza kwa watu wengi hasa vijana wenye nguvu kabisa. Yaani hivi sasa kuna watu ambao watashinda kutoka asubuhi mpaka jioni kwenye facebook au instagram bila kufanya kazi yoyote yaani myu ataamka asubuhi kabla hata ya kufanya kiyu chochote aingie kwanza kwenye mitandao ya kijamii ndo asikie raha kitu ambacho hakileti maendelea yoyote.

5. Kuvunjika kwa Mahusiano 

Kwa kiasi kikubwa mitandao ya kijamii imepelekea kwa mahusiano mengi sana kuvunjika yaani watu wengi wanaitumia vibaya hii mitandao, zamani ilikuwa ili upate mchepuko basi ukakutane mtu mbali huko lakini siku hizi unakutana na mtu kwenye kiganja cha mkono wako hivyo imerahisisha zaidi watu kupata michepuko na kuvunjika kwa mahusiano mengi sana, hasa hawa wasichana wanaopiga picha za nusu uchi watu wanajikuta wanaharibu mahusiano

Ingawa Mitandao ya Kijamii ina faida nyingi hizi ni baadhi tu ya hasara za kuwepo kwa mitandao ya kijamii hasa kwa hizi nchi zetu za Afrika.

Je kuna hasara nyingine ambazo sijazitaja tafadhali funguka hapo chini na uonhezee za kwako

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.