Harmorapa awataja mastaa ambao waliompa jina analolitumia sasa

Image: Harmorapa

Rapper wa Tanzania, Harmorapa, kwa sasa hivi ni mmoja wa watu maarufu Afrika Mashariki. hii ni kwa sababu ya jina lake na pia nyimbo anazoziachilia.

Kabla ya kuwa staa mkubwa rapper huyo hakuwa anatumia jina hilo lakini baada ya kujitokeza na alikutana na mastaa kadhaa waliomshauri kutumia jina analotumia sasa.

download latest music    

Akizungumza katika show ya Bongo Dot Home cha Times FM, Harmorapper alisema kuwa Roma na Mr T-Touch ni watu ambao walimsihi kutumia jiona la Harmorapa na pia kwa sababu anafanana na mwimbaji wa Wasafi records, Harmonize

“Baadhi ya mastaa wakubwa katika muziki wa hapa Bongo nao walinishauri nijiite hivi, akiwemo brother Roma Mkatoliki na Mt T-Touch,”

Hapo mbeleni rapper huyu wa Tanzania alikuwa akifahamika kama Jembe la Kusini, jina ambalo ata mimi kama shabiki wake naona halingeweza kumake kwa hii industry.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua