Hili ndilo jibu Babu Tale Meneja wa Diamond alimpa Waziri wa Utalii baada ya kuwaambiwa atangaze Tanzania bure

Ikiwa kuna biashara Diamond Platnumz anadai kuinyakua, ni ile ya kutangaza nchi yake lakini wizara ya utalii haiko tayari kumpea hela zozote kufanya hiyo kazi.

Na waziri Prof. Jumanne Maghembe alihakikisha jambo hilo alipomjibu meneja wake Babu Tale. “Wasanii wetu wenye majina makubwa watangaze tu Tanzania, Tanzania ni nchi yao sio lazima mpaka waambiwe waje tukae pamoja  tupange mikakati na tuangalie ni kitu gani anaweza kufanya na watusaidie kutangaza utalii wetu” alisema.

download latest music    

Hapo ndipo Babu Tale alijibu kwa kueleza hivi:

“Duh hapa sijui mimi mshamba au sijamuelewa vizuri Mh Waziri kuhusu kuitangaza Tanzania mimi kwa akili yangu fupi naona watu wa nchi jirani wanatafuta wasanii watanzania kutangaza nchi zao hapa kwetu tunaambiwa tuombe ili tutoe msaada mh sasa hela ya wizara inaenda wapi???? >>>>> Babu Tale

“Cha ajabu unaweza ukaambiwa uitangaze nchi halafu utapelekwa mbugani bure duh. Ninachojua kila sekta inamfuko sasa hili eneo la utalii mfuko upo wapi mimi naendelea kuuliza mfuko wa kuitangaza Tanzania kwa nia nzuri na mazuri yaliyopo umewekwa wapi??>>> Babu Tale

“Leo wasanii wengi wanakimbilia hata kufanya video zao nje ya nchi sababu ukitamani kufanya kitu nchini inakuwa kama mtu anakukomoa usifanye. Hvi Samatta anavyofunga magoli wangewaza kumvalisha bendera ya tanzania nguo yake ya ndani pale anapofunga goli avue watu waone duniani kuna nchi inaitwa Tanzania ingekuwa je?>>> Babu Tale

“Sina nia mbaya ila tuamke kweli kuitangaza nchi yetu na sio wahusika waifuate sekta husika wakati kila sekta inakitengo cha matangazo na wanajua nani wakupewa jukumu #mtazamochanya #Tanzania #”

About this writer:

Irari Ngugi

Lover of life, lover of big boobs and certified celebrity squasher. Catch me if you can on facebook as Irari Ngugi