Huu ndio ujumbe Rapper Jay Moe aliutoa kwa wanamuziki wote wa Nje

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, rapper Jay Moe amejitokeza na kuongelea mambo mbali mbali kuhusu muziki Tanzania.

Alizungumzia kwanza uwezo wake wa kuandika nyimbo na kugusia nyimbo ambazo ameziandika Tanzania moja wapo ikiwa Aseme wa Q Chilah.

download latest music    

Pia alisema angetaka sana kumwandikia Bill Nass wimbo.

Moe amekiambia kipindi cha On The Eight cha TVE kuwa hawezi kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka nje mapaka atakapokuwa na video walau tano ambazo msanii huyo ataweza kuziangalia na kuufahamu uwezo wake zaidi tofauti na ilivyokuwa sasa bado hana video za kutosha.

Hitmaker huyo wa Pesa Madafu ameongeza hata alipokuwa Afrika Kusini mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini P-Funk Majani alimpigia simu na kumtaka kushoot video huko lakini alimwambia kuwa yupo huko kwa ajili ya kushoot video moja ya kutimiza miaka yake 11 bila ya kuwa na video nyingine.

Jay amesisitiza kuwa akifikisha video za kutosha itakuwa ni vizuri kwake hata zikichezwa kwenye vituo vingine vikubwa vya nje ya nchi ikiwemo Nigeria. Rapper huyo kwa sasa ameachia video yake mpya ‘Nisaidie Kushare’ baada ya wimbo wake wa ‘Pesa Madafu’ kufanya vizuri kwenye redio na runinga.

About this writer:

Irari Ngugi

Lover of life, lover of big boobs and certified celebrity squasher. Catch me if you can on facebook as Irari Ngugi