Joh Makini: Davido alinifwata kutafuta collabo na mimi

Joh Makini aliwaahidi mashabiki wake kufanya collabo kubwa na Davido – msanii anayetajika sana nchini Nigeria na barani Afrika.

Davido alidhibitisha collabo yake na Joh Makini kupitia mitendao ya kijamii. Kwenye Instagram yake, Davido alipost  picha akiwa pamoja na Joh Makini na kuandika maneno yalisomeka “Back to work On set shoot @johmakinitz ft Davido ….. TZ  x NAIJA”

download latest music    

Joh Makini amefunguka na kueleza kuwa Davido ndiye aliyemfwata na kupendekeza wafanye collabo – wengi walikua wanadhani Makini ndiye aliyemwomba Davido kushirikiana naye kimuziki.

“Mimi naona ni kwasasabu alikuwa excited sana kufanya kazi na mimi, halafu wakati wa kufanya hii ngoma yeye ndiye aliyekuwa wakwanza kuniapproach mimi. Kwa hiyo nafikiri ni mtu ambaye alinifuatilia na akaupenda muziki wangu ndiyo maana hata chemistry imekuwa nzuri na tumefanya kitu kikubwa,” Joh Makini alisema.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere