Juma Nature akana kumlipisha Harmorapa kufanya kolabo naye

Wiki chache zilizopita, rapper mpya kwenye sanaa ya muziki Harmorapa alilalamika kuhusu wasanii wakongwe kuwalipisha wasanii wapya wanapotoa kolabo nao.

“Haipo sawa kwa wasanii wakubwa kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati wanajua bado hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe,” Harmorapa alisema.

download latest music    

Juma Nature, aliyetoa kolabo na Harmorapa, alikana kuwa alimlipisha Harmorapa kufanya kolabo naye. Akiongea na kipindi cha E News cha EATV, Juma Nature alisema Harmorapa hana pesa ya kumlipa.

“Nikisema nimemlipisha Harmorapa pesa kwa ajili ya kolabo nitakuwa nakosea. Mimi ni mtu mzima nilikubali kufanya wimbo na msanii yule kwa sababu ni mkali na anajua muziki pia na imani atafika mbali. Hawezi kunilipa mimi, ana hela gani?,” Juma Nature aliambia EATV.

Harmorapa

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere