Kimeumana! Wema Sepetu amkana rafiki wake wa dhati Zena Abdallah

Wema Sepetu na rafiki wake wa karibu Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ sasa hawana uhusiano mwema baina yao tena. Hii ilibainika baada ya mdau mmoja kuweka picha ya Jike Shupa wakiwa pamoja na Wema na kusema ni marafiki.

Wema alijibu kwa upesi na kumkana Jike Shupa hadharani kwamba siyo rafiki yake.

download latest music    

“Wema kafuta urafiki na James Delicious sasa hivi kaunda urafiki na msagaji Jike Shupa, dada una marafiki wabovu hawaendani na hadhi yako, angalia wewe…,” aliandika mdau huyo.

Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ na Wema Sepetu

 

Risasi Jumamosi inaeleza kwamba uhusiana baina ya Wema na Jike Shupa uligonga mwamba kutokana na watu kuzungumza mengi kuhusu Jike Shupa huku wakimkataza Wema kuendelea kuwa na ukaribu naye kwa kile wanachodai kwamba tabia zake siyo nzuri.

“Watu wamekuwa wakimpigia Wema kelele za kuacha ushosti na Jike Shupa kwa sababu ya tabia zake maana kila mara amekuwa akionekana akifanya vitendo vya ajabu hadharani kama kunyonyana ndimi na wanaume tofautitofauti, kubadili wapenzi kila kukicha huku akihusishwa pia na usagaji,” Risasi Jumamosi iliripoti.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere