Lady Jay Dee afichua kinachomfanya ku-hit kwa miaka 17 sasa

Jay Dee amesisitiza kuwa mafanikio yake kwenye muziki ulipigwa jeki na hatua aliochukua miaka kumi na saba iliopita.

Mwanamziki huyo anasema kuwa kitendo cha yeye kutolewa na sifa ndiyo kimemfanya kuendelea ku-hit katika sanaa ya muziki.

download latest music    

Jay alisema wasanii wengi hupotea baada ya kuwa staa na kushindwa kutoa nyimbo zingine kwa sababu ya kulewa na sifa.

Msanii huyo alifichua kwamba kutolewa na sifa ndiyo siri pekee iliyomfanya aweze kupita katika vipindi vyote vigumu maishani mwake.

“Ukifanya ngoma na watu wakakujua utakuwa staa lakini usilewe sifa ukilewa mapema utalala alafu utashindwa kuamka…ni miaka kumi na saba sasa, sijawahi kulewa na kila siku naona kama nahitaji kujifunza kitu kipya” Alisema Jay Dee.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere