Linah adai wazazi wake walimkataa mpenzi wake kwa sababu ya dini

Image: Linah

Linah ambaye ni muimbaji maarufu Tanzania amefunguka mara ya kwanza kuhusu mchumba wake na baba ya mtoto anayemtarajia hivi karibuni.

Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds Fm alisema kuwa dini iliwafanya wazazi wake kumkataa mchumba wake mara ya kwanza. Muimbaji huyo alisema kuwa amelelewa katika misingi ya dini ya kikristo na alipopata mimba ya mwanaume wa dini nyingine iliwafanya wazazi wake kuwa na ugumu wa kumkubali mwanaume huyo.

download latest music    

“Mwanzoni wazazi wangu walimkataa mpenzi wangu kisa ni dini tofauti na mimi, lakini sasa hawana pingamizi. Tumeunganisha damu na kwenye mahusiano naamini upendo, nisingependa mtu anipangie, lakini jambo la wazazi kwa familia za kiafrika ni tofauti.”

Aliendelea kusema kuwa hajuti kubeba mimba hiyo kwani aliipata at the right time.

Nimebeba ujauzito katika right time kwangu na mwenzangu yupo tayari. Mashabiki wategemee ndoa kabisa muda wowote.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua