Mashabiki wa King Kiba wamtolea Barakah the Prince hasira baada ya kumpost Chibu

Image: Baraka

Ingawa Baraka the Prince alifanya wimbo na King Kiba Nisamehe haamanishi kuwa hawezi msupport Diamond Platnumz. Hata hivyo hivi sivyo mashabiki wa Kiba wanavyofikiria. Hivi Karibuni muimbaji huyu wa Bongo, Baraka the Prince aliupost wimbo mpya wa Diamond Platnumz na kilichofuatia ni matusi kutoka team Kiba.

Soma: Baada ya kufanya collabo na King Kiba, Barakah The Prince aeleza changamoto alizopitia

download latest music    
Barakah The Prince
Barakah The Prince

Mashabiki wengi ambao wamekuwa wakicomment kwa picha hii wanashangazwa na Baraka kupost wimbo huu kwa sababu wengi wanajua Baraka yuko kwenye lebel moja na Alikiba.

Kama mnavyoelewa Kiba na Diamond wamekuwa na beef kwa muda sasa kwa hivyo Baraka asingeweza kupost chochote kuhusu Diamond Platnumz, wengine wamecomment kwa kutopendezwa na post hiyo wengine wamepost kumpongeza.

Kupitia Instagram Barakah the prince aliandika kusema…

Chanzo cha kutengenezewa maden na makaka poa..ila mama alinifunza kukaa kimya..eeehh mungu niokoe vita

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua