Maswali Unayoweza Kumuuliza Mpenzi Wako Mara Ya Kwanza Mnapokutana

Watu wengi wanakuwa na kigugumuzizi kwa mara ya kwanza anapoenda kukutana na mtu anaempenda, wapo wengine hujikuta wanapata muda mgumu dakika chache kabla ya kukutana na mtu kabla ya kukutana na kuanza kujifikiria ni kitu gani ataenda kuongea anapoenda kukutana na mpenzi wake.Basi usipate shida, haya ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kumuuliza mpenzi wako kwa mara ya kwanza mnapokutana ingawa unashauri usiyakariri ukajikuta unataka kumuuliza kwa mpangilio, kwanza atakushangaa na kukuona wewe ni muoga.

Hii ni kwa wanaume zaidi ambao mara nyingi first-date wanapaswa kuwa dominant wa mazungumzo, ili yule unaendaa kukutana nae aweze kukukubali.

download latest music    

1.Umeipenda sehemu hii,

Inawezekana ni outdoor dating ,umeamua kumpeleka sehemu fulani, jitahidi kumuuliza kama ameipenda sehemu hiyo, na kama ameipenda amependa nini zaidi, kwanini ameipenda au kwanini hajaipenda.na kama hajaipenda basi muulize angependa kukaa sehemu ya aina gani tofauti na hiyo.

2.Huwa unapenda kunywa au kula nini,

Huu pia ni mwanzo wa kujua ni kitu gani huwa napendelea zaidi, kadri anavyoweza kufunguka ndivyo itakusaidia wewe kumjua kiundani zaidi.kuna baadhi ya maswali hayawezi kuulizwa moja kwa moja lakini kupitia swali moja unaweza kujikuta unapata jibu ya swali lingine, kwa mfano utakapomuuliza kuhusu chakula unaweza kujua pia kama anajua kupika au kufanya shughuli ndogondogo za nyumbani.

3.Nyimbo  au movies gani unapendelea Kuangalia

kuwa na hamasa ya kujua partner wako anapendelea aina gani ya muziki au movies gani anapendelea zaidi , kwanini anapendelea aina hiyo, je kuna historia yoote inayompelekea kupendelea aina hiyo ya muziki kama ipo basi mchimbe taratibu  na atafunguka bila wasiwasi.

4.Unapendelea kufanya nini muda wake wa ziada,

hii pia itakusaidia wewe kujua ni muda gani unaweza kuwa na muda wa mpenzi wako pia,sio kila saa uanmuuliza mpenzi wako anafanya nini au yuko wapi,atakapofunguka kuhusu muda wake wa ziada anafanya nini inakupa nafasi pia ya kupanga ratiba zako vizuri ili kuwa nae mara nyigine.

5.Unapenda nini kwa mwanaume au rafiki yako wa karibu,

nadhani hapa watu wengi hukosea kwa sababu ujikuta nanmuuliza mpenzi wake moja kwa moja kuhusu yeye, jaribu kumtega ili afunguke zaidi kwa sababu inawezekana akijibu kuhusu wewe hatokuwa huru zaidi au wewe unakuwa -disappointed na majibu yake.

6.Nani ni mtu wako wa karibu katika familia yako, kwanini? ,

ni vizuri zaidi pia kujua mahusiano ya mpenzi wako na watu wake wa karibu, kwa sabau swali hili pia linaweza kumfanya akawa wazi hata kuelezea kwa undani malezi yake na familia yake kwa ujumla hivyo itakusaidia kujua mtu gani unaingia nae katika mahusiano.

7.Jaribu kumsifia kuwa amependeza ikibidi muulize kigzo gani alitumia kuchagua kivazi icho kwa siku kama iyo ya kukutana na wewe,hii itakuwa imekaa sana kwa wakaka.swali hili litakupelekea kujua pia aina ya nguo anazopendelea kuvaa  na style yake ya maisha kwa ujumla.

Kuna baadhi ya maswali hayakai vizuri kama utamuuliza mpenzi moja kwa moja  wako kwa mara ya kwanza , isipokuwa labda yameingilia tu katika maongezi au katika njia ya ucheshi, haya yanaweza kuwa kama:

-Mara yako ya kwanza kupenda ilikuwaje, ulikuwa na umri gani.

-Ni sehemu gani ya mwili wako iko sensitive kuliko nyingine.

-Ni nini uwa mnafanya au kuongea  unapokuwa na marafiki zako wa kike.

-Kwa muonekano wangu leo ninaweza kuwa mtu wako wa karibu.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.