Mkubwa Fella: Hakuna msanii aliyekatazwa kuondoka ndani ya kundi ya Yamoto Band

Mkurugenzi wa Yamoto Band Mkubwa Fella amefunguka kuhusu utata ambayo umekumba bendi hio baada ya Aslay kutoa wimbo wake binafsi.

Uvumi ulienea kuwa Aslay alizuiliwa kuondoka kundi hilo baada ya kufanya project yake ya muziki ya kibinafsi bila kushirikisha bendi ya Yamoto.

download latest music    

Akiongea na Bongo5, Mkubwa Fella alieleza kuwa wanabendi wa Yamoto wako na uhuru wa kuondoka ndani ya kundi hilo wakati wowote.

Mkubwa Fella

Fella pia alisema wasanii wa Yamoto wako na uhuru wa kufanya project zao binafsi za muziki.

“Hakuna msanii ambaye amekatazwa kuondoka Yamoto Band hata Mkubwa na Wanawe ila ukiondoka bila kuaga haufiki sehemu yoyote.

“Mimi nawasaidia kuwaonyesha njia wafike sehemu fulani, mtu akijiona amekuwa kwanini nimzuie?. Hakuna aliyefungwa kwa namna yoyote, sema ni vyema mtu kufuata taratibu hata za makuliano yetu ya mdomo.

“Aslay hivi karibuni ameachia kazi yake mpya na sisi tunamsupport kwa sababu kabla ya Yamoto Band, Aslay alikuwa msanii ila sisi tulimtumia yeye kuwainua wenzake na kweli tumefanikiwa leo hii vijana wanapata makate wao wa kila siku. Kwa hiyo hata wasanii wenzake wanaweza kufanya hivyo pia lakini kama wanamakubaliano yao binafsi siwezi kuyaingilia,” Mkubwa Fella alisema.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere