Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers amlenga Ali Kiba baada ya kumkosoa Babu Tale

Eric Shigongo, mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, alianza mgogoro na Wafasi alipodai kuwa Diamond anaingizwa shimoni na Naseeb Abdul, Babu Tale na Salaam.

Madai yake Shigongo yalimkera sana Babu Tale na kumlazimu kumwonya kutoingilia biashara yake na kuwachafulia jina wasanii wake.

download latest music    

Soma pia: Meneja wa Diamond Babu Tale amrarua mmiliki wa kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo

Mfanyabiashara huyo sasa amefunguka na kuamua kumshauri Alikiba kuhusiana na muziki wake na namna ambavyo anatakiwa kuishi kwa mipango ili hata siku asipokuwepo kwenye ramani ya muziki awe na maisha yenye tija kulingana na kazi alizofanya nyuma.

“Kwanza kabisa nianze kwa kukiri kuwa sikuwahi kukutana na Alikiba ana kwa ana mpaka miezi miwili iliyopita nikiwa katika Hotel ya Double Tree, iliyopo Masaki, Jijini Dar es salaam. Nilikwenda pale kwa ajili ya chakula cha mchana na mke wangu. Muda mfupi tu baada ya sisi kuingia walifika Alikiba na meneja wake Christine Mosha (Seven) wakaja moja kwa moja kwenye kona tuliyokaa na kutusalimia. Kitu cha kwanza nilichojifunza na kukipenda kwa Alikiba ni unyenyekevu, kijana huyu ni mnyenyekevu mnoooo! Kitu hiki peke yake ukiachana na muziki wake kilinifanya nimpende Kiba. Walipoondoka mimi na mke wangu wote tulikiri KIBA NI MNYEYEKEVU NA NDIYO SABABU AMEFANIKIWA SANA KATIKA MUZIKI.

Shigongo

“Alikiba, meneja wake na Watanzania wenzangu lazima mnisikilize hapa; MAFANIKIO MAISHANI HUJA NA KITU NYUMA YAKE, mara nyingi kitu hicho huwa kuwapuuza na kuwadharau waliokufikisha ulipo. Kuwatenga bila kufahamu hao ndiyo wanunuzi wa kazi zako ama wasikilizaji wa muziki wako na wakikuachia tu utatumbukia shimoni na huo ndiyo utakuwa mwisho wako. Ali kiba anapaswa kufahamu kwamba hawezi kuwa Champion for life, hata akiwa bora kiasi gani lazima siku moja atakuja mtu bora zaidi yake. Kabla ya Chris Brown alikuwepo Usher Raymond, kabla ya Rihanna alikuwepo Beyoncé, kabla ya Floyd Maywether alikuwepo Mike Tyson, kila zama na bingwa wake. Leo ni Kiba kesho atakuwa mwingine” alisema Shigongo.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere