Msanii Barnaba adai kuwa ni bora fedha zao za muziki ziibiwe na Diamond

Hitmaker  wa ‘Lover Boy’ anadai kuwa ni bora wasanii waibiwe na Diamond Platnumz kuliko kuibiwa na mtu binafsi ambaye si mwanamziki.

Barnaba amemsifu Diamond kwa kuanzisha tovuti yake ya kuuza muziki ya Wasafi.com. Msanii huyu alikutana na Diamond alipomtembelea katika ofisini kwake.

download latest music    
Barnaba na Diamond

“Tumeibiwa sana wasanii, tumedhulumiwa sana. Mungu anisamehe kidogo, bora atuibie msanii mwenzetu, tunajua msanii mwenzetu anakula yupo kwenye soko letu kuliko atuibie mtu binafsi.”

““Na yeye akiwa kama CEO [Diamond] alichukua uamuzi wa busara kama heshima kutupigia simu wasanii wenzake mwenyewe kuliko kuwatuma menejimenti. Mimi naona jambo zuri la bahati alilolifanya na nilienda nikachukuwa contract yangu na kiukweli nimeusaini lakini bado kuurudisha,” Barnaba aliambia Dizzim Online.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere