Msanii kutoka Wasafi Harmonize azungumza mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na Wolper

Msanii Harmonize juzi alikuwa kwenye Clouds fM na alizungumzia mambo mengi kuhusu wimbo wake na sana sana kuhusu uhusiano wake na Wolper.

Harmonize aliulizwa na Mami baby kama ilikuwa kiki au nini baada ya kudaiwa kuachana na Wolper na ukaribu wao kurejea leo wakati anaachia wimbo wake mpya.

download latest music    

Harmonize

“kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi ila sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na Mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki nilianza naye nikiwa sina hata gari”  Harmonize alieleza.

Alihakikisha lakini hawakuwa pamoja;

“Ukiona mtu anatumia nafasi yako kuvuma ni jambo la kumshukuru Mungu, sikatai yupo kwenye miahangaiko atatoka, Mungu amjalie najua wote tunatoka kwenye familia za kimaskini ni wakati wake sasa kuonyesha alichojaliwa” Alimtakia Wolper kila la heri.

About this writer:

Irari Ngugi

Lover of life, lover of big boobs and certified celebrity squasher. Catch me if you can on facebook as Irari Ngugi