Mwigizaji wa filamu Batuli afunguka kuhusu beef yake na Irene Uwoya

Image: Batuli

Yobnesh Yusuph anayejulikana kwa umaarufu kama ‘Batuli’ amedai kuwa yeye hana beef yoyote na mwigizaji wa kibongo, Irene Uwoya. Mwigizaji huyo aliendelea kusema kuwa Uwoya ndiye anapaswa kueleza beef yao inatokana na nini kwani yeye ndiye anayesambaza maneno haya.

Batuli
Batuli

Batuli aliendelea kusema kuwa hana muda wa kuanzisha ugomvi na mtu yoyote haswa Uwoya. Kulingana na yeye amewazibia watu macho na maskio wanoeneza stori hizi mitandaoni. Batuli alisema,

download latest music    

“Sina muda wa kugombana na Uwoya, kama kuna tatizo aulizwe yeye siwezi kuusemea moyo wake.”

Uwoya
Uwoya

Uwoya alipotafutwa kupitia simu yake Mwigizaji huyu hakushika wala kujibu SMS kuhusu beef hii yake na Batuli. Kwani kuna nini?

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua