“Naona amepanga kunichafua” Rayvanny amkana Mishi Dorah anayemdai kimapenzi

Rayvanny aliyekuwa nchini Kenya hivi majuzi amekana Mishi Dorah amabaye ni mwanake wa makamo na bado anamtaka Vanyny boy kimapenzi.

Staa huyu wa tanzanian amefunguka kwa kusema kuwa amekataa ofa za Mishi Dorah ambaye anaonekana kumharibia jina nchini Kenya na sasa pia Tanzania. Mishi ambaye ni mwigizaji wa reality show amekuwa akitangaza kuwa ashawai kuwa na Rayvanny kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, wiki iliyopita. Aliskika akisema,

download latest music    

“Ninampenda Rayvanny, nitamtafuta kwa udi na uvumba nimtunuku penzi ili roho yangu itulie, nampenda sana kwa kweli,”

Mishi Dorah

Ata hivyo Rayvanny sasa amefenguka huku akisema kuwa amekuwa akiona anachosema Mishi Dorah, lakini hatakai mambo ya mwanamke huyu kwani anahofia nyumba yake kuvunjika na pia brand yake kuharibika. Akizungumza Rayvanny alisema,

“Yaani sitaki kumuongelea kabisa huyo mwanamke, maana naona amepanga kunichafua kwani nilienda Kenya wakati f’lani nikakuta habari zake, huku nyumbani Bongo ndiyo hivi tena, sina cha kuongea maana mtu akiamua kukuchafua huwezi kuongea kitu.”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua