Nay Wa Mitego: Mwambieni Diamond pia awe mpole kwasasa alee watoto

Nay Wa Mitego amezua hisia tofauti baada ya kumpasha Rich Mavoko ujumbe ambao alitaka uwafikie wasanii wote wa Wasafi Diamond akiwepo.

Rich Mavoka aliandika kwa ukurasa wake wa Instagram kutambulisha wimbo wake mpya ambayo bado haujaachiliwa kwenye redio na runinga.

download latest music    

“Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ? #Showme” Rich Mavoko aliandika.

Nay Wa Mitego alimjibu haraka, alimwambia asubiri mbaka mwakani 2018 ndo watoe nyimbo (wasanii wa Wasafi.) Alimwambia apitishe ujumbe kwa Diamond ambaye alimtaka alee watoto kwanza.

Nay Wa Mitego na Diamond

“”NAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI. MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWASASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA✊?. Wimbo wetu wa TAIFA ni #Wapo LINK ON MY BIO☝”,”Nay Wa Mitego aliandika.

Ujumbe wa Nay Wa Mitego hata hivyo ni utani tu, Diamond ni rafiki wake mkubwa ambaye alishirikiana naye kutoa ngoma kali sana ‘Muziki Gani’.  Si mara ya kwanza wawili hao kutupiana vijembe kupitia mitandao.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere