New Video: Harmonize aachia video yake mpya aliyomshirikisha mpenzi wake kama video vixen

Image: Harmonize na Wolper

Msanii wa Tanzania Harmonize ameachia mpya video ya wimbo wake mpya Niambie aliofanya miezi 6 baada ya Matatizo.

Harmonize ambaye anafanya kazi chini ya uongozi wa Wasafi records amefurahisha washabiki kwa wimbo huu uonawagusa kidani maana ameimba kuhusus mapenzi, kitu ambacho mashabiki wa bongo hupenda.

download latest music    

Katika video yake, Harmonize alimshirikisha mpenzi wake wa dhati, Jacqueline Wolper. Kwa kufanya hivi, mashabiki wengi wameachwa wakifikiria kuwa mapenzi yake na Wolper ni ya kiki.

Hata hivyo, alifutilia maneno haya mbali alipokiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii, kuwa kuna wakati alipogombana na mpenzi wake lakini sasa wamesuluhisha kila kitu.

“Kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa, lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi. Sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki,”

Hata hivyo, tazama video yake mpya hapa.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua