Paul Makonda asema vijana wengi wameacha madawa ya kulevya tangu awachukulie watu maharufu hatua

Image: Paul Makonda

Paul Makonda anaonekana kuwa mtu anayefuraha nyingi baada ya kufanya vijana waache kutumia madawa ya kulevya. Katika sherehe zilizofanyika hivi majuzi, Paul Makonda alisikika akisema kuwa vijana wengi wameacha madawa kupitia jitihada alizofanya kwa kushirikiana na Watendaji wengine wa Serikali.

Soma:“Mkome kunihusisha na watu wasio jua kitu chochote kuhusu maisha yangu” Wema Sepetu awaonya mashabiki
Mh Makonda huyu amesema kuwa jambo hilo linawafurahisha wazazi wengi walikuwa wanahofia watoto wao kupotea kwa kutumia madawa haya. Ingawa si wote wamebadilika, Makonda anaendelea kujitia moyo kuwa siku itafika na pia wao watanaswa na mkono wa serikali kuwanyosha.

download latest music    

Mwezi uliopita Paul Makonda aliwapeana amri kuwa Wema Sepetu, Romy Jones, TID na wengine wakamatwe kwa kushukiwa kuwa walikuwa wanahuika na mauzaji na matumiaji ya dawa za kulevya.

Lakini kwa sasa Paul Makonda amemsifu TID kwa kusema kuwa anaendelea vizuri na pia afya yake inaendelea kuwa nzuri. Hivi sasa anvutia kisura na ikiwa amejitolea kuachan madawa kabisa, basi mwezi ijayo atakuwa mtu wa maana tena

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua