R.I.P English! Shilole sasa asema kuwa hapendi kuzungumza lugha ya Kiingereza pasipo sababu

Msanii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameoneka akizungumza Kiingereza kibovu kwenye video ambayo imesambaa sana kwenye mtendao wa kijamii.

https://www.youtube.com/watch?v=p9KUgS4_oOY&feature=youtu.be

download latest music    

Lakini ata hivyo msanii huyo amedhibitisha kwamba ako na umaarufu wa kuzungumza lugha ya Kiingereza. Shilole anasema kuwa yeye hawezi kuzungumza Kiingereza pasipo na sababu.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Shilole alisema watu wanaomtaka yeye kuzungumza Kingereza wanapoteza muda wao kwa kuwa yeye alijifunza lugha hiyo kwa ajili ya maslahi yake binafsi hasa katika biashara zake.

“Mimi lugha naijua sana, nimesoma kozi ya miezi mitatu, mwalimu alikuwa anakuja nyumbani kwangu kunifundisha, ukitaka kujua mimi najua kuzungumza lugha hiyo unikute kiwanja cha ndege nimechelwa ndege halafu nina show au ninapokuwa mezani nataka kuzungumza na wazungu kwa ajili ya kusaini mikataba lakini siwezi kuongea kwa kila mtu ili kudhihirisha kama naweza kwakuwa hakuna aliyenisaidia kulipa ada”, alisema Shilole.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere