Rayvanny afunguka kuhusu collabo yake na Bahati

Collabo ya Rayvanny na Bahati imeweza kupata umaarufu kwa siku chache baada ya kuachiliwa na Wasafi records. Wimbo huu ambao ni wa Injili umempa Bahati uwezo wa kupenya Tanzania na Kenya pia na kulingana na alichosema sema Diamond Platnumz wawili hawa wanaenda mbali kimuziki.

Hata hivyo Rayvanny hivi karibuni alifunguka kuhusu collabo hii na kulingana na alivyoongea, kijana huyu hana majuto yoyote kumchagua Bahati kama msanii ambaye angefanya project na yeye

download latest music    

Akiongea katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM Jumanne hii, Rayvanny alisema kuwa kabla ya kuanza kuimba alianza kuimba kwaya kanisani.

“Kwanza mimi nimekuwa nikimfuatilia Bahati kwa muda mrefu na nilikuwa nikifikiria nikikutana naye nitaimba wimbo wa aina gani na mimi niliwa narap huko nyuma lakini nimejua kuimba kwa kupitia kanisani. Kwa hiyo haikuwa ngumu kwangu kufanya kwa sababu ni wimbo wakijamii zaidi ndio maana wimbo hauonyeshi kama ni wa Injili au wakidunia,”

Sasa hivi wimbo wao wa nikumbuke umeweza kupata airplay mzuri katika nchi zote mbili.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua