Rayvanny afunguka kuhusu namna alivyoweza kushirikiana kimuziki na Bahati – muimbaji wa Gospel kutoka nchini Kenya

Watu wengi walishangaa baada ya Rayvanny and Bahati kutangaza kuwa wameshirikiana kimuziki, wawili hao walitoa wimbo unaoitwa ‘Nikumbushe’.

Rayvanny sasa ameeliza namna alivyoweza kushirikiana kimuziki na muimbaji huyo wa nyimbo za injili kutoka Kenya.

download latest music    

“Kwanza mimi nimekuwa nikimfuatilia Bahati kwa muda mrefu na nilikuwa nikifikiria nikikutana naye nitaimba wimbo wa aina gani na mimi niliwa narap huko nyuma lakini nimejua kuimba kwa kupitia kanisani. Kwa hiyo haikuwa ngumu kwangu kufanya kwa sababu ni wimbo wakijamii zaidi ndio maana wimbo hauonyeshi kama ni wa Injili au wakidunia,” Rayvanny alisema akiongea katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM.

Tazama ‘Nikumbushe’ kwenye video hapo chini:

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere