Shigongo aelekeza mawaidha yake kutoka Diamond na kuipelekea Ali Kiba..hivi ndivo alivyo mshauri kuhusu wazazi wake

Mmamiliki wa Global publishers bado anaendelea kutoa mawaidha yake kwa wasanii wa Tanzania.

Alianza na Diamond ambapo alitukatanwa na mashabiki na sasa ako kwenye Ali Kiba ambapo alizungumzia mambo mengi mpaka ile ya kifamilia.

download latest music    

Hivi ndivyo alivyomweleza Ali Kiba:

1. ‘Detachment from fans’, hii ina maana ya kujitenga kutoka kwa mashabiki zake. Linaweza kuonekana kuwa jambo dogo lakini limekuwa likiwaangusha wanamuziki wengi duniani. Hili ni la kwanza ambalo anatakiwa kujiepusha nalo kama atataka kuwa juu kwa kipindi kirefu.
2. Ali ni mnyenyekevu, hataki makuu lakini kwa kazi yake ilivyo inambidi kidogo aongeze thamani, hapa nina maana kwamba Ali ajiepushe na suala la kusafiri bila meneja anapokuwa ndani au nje ya nchi kwenye shoo. Simaanishi kwamba hasafiri naye, hapana, namaanisha kwamba asifikirie kutokusafiri naye kwani hii huongeza thamani ya msanii anapoongozana na timu yake, hasa meneja au mameneja.

3. Asiyumbishwe na ushindani. Huu upo kote duniani na ndiyo maana ni rahisi kusikia Nicki Minaj anashindana na Iggy Azalea. Anachotakiwa ni kuweka chapa zake katika aina fulani ya muziki ili vizazi vijavyo viweze kumkumbuka kwa muziki wake fulani kama anavyojulikana Michael Jackson kwa muziki wa Pop.

4. Afanye sana kazi za kijamii. Hili linaonekana kuwa jambo dogo sana lakini unapoamua kufanya kazi za kijamii inakuweka karibu na mashabiki zako na pia unabarikiwa kulingana na kile unachokifanya.
5. Asiweke nguvu zake nyingi katika mambo yasiyokuwa na tija. Hili huwa linamfanya mwanamuziki kupotea haraka. Skendo hazikufanyi kusikika bali zinakufanya kupotea kwani mashabiki zako watakuwa wanahitaji muziki, hawahusikii inavyotakiwa, skendo zinakuwa nyingi kuliko kazi. Kiba amejulikana kwa sababu ya muziki, hajajulikana kwa sababu ya skendo, waliosikika kwa skendo acha wafanye skendo ila kama umejulikana kupitia muziki, fanya muziki.

6. Awasaidie wazazi wake kwa kila kitu. Wazazi ndiyo nguzo muhimu sana hapa duniani. Unaweza kuona unafanikiwa lakini unapomwacha mzazi ni lazima kutakuwa na vitu vibaya vitatokea, huwezi kuviona sasa hivi, kuna siku ukishaanza kushuka, kuna sauti moja ya upole itasikika moyoni mwako, itakwambia kwamba tatizo halikuwa kukosa thamani, halikuwa kukosa mapromota, tatizo kubwa lilikuwa ni mama au baba kwani Mungu aliwachagua hao wawe wazazi wako kwa makusudi yake.

7. Nilipokutana na Seven na kuzungumza naye, nilibahatika kumwambia kuhusu gharama kubwa, kwa unyenyekevu mwingi, alikiri kuwepo kitu hicho na ndiyo maana shoo zake si nyingi sana nyumbani. Namnukuu Seven: “Ni kweli Eric, gharama zipo juu lakini ndivyo tunavyotoza hata huko nje. Ili kidogo tufanye shoo za kutosha hapa nyumbani, basi wadhamini wajitokeze wengi japo na sisi gharama zishuke kwa kuwa wakijitokeza wengi, na sisi tutaingiza kingi hivyo hata malipo yatakuwa madogo. Kama akija mdhamini mmoja, inajulikana kwamba lazima shoo iwe ya gharama sana. Lakini mbali na hilo Eric, naandaa kufanya shoo za hisani mara kwa mara ili kuisaidia jamii kwani naamini itamfanya Ali kuwa karibu na mashabiki zake.”

Aliendelea kuongea kwamba malipo ya nyumbani yana kila sababu ya kushushwa kwa kuwa Tanzania ipo chini kiuchumi, si kama Afrika Kusini au nchi za Ulaya. Mashabiki watuelewe tu kwamba tunajua kwamba wanatofautiana kifedha, hatuwezi kuwatenga kwa kuwa wote ni mashabiki zetu, tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha shoo zinamfikia kila mtu,” alimalizia Seven.

About this writer:

Irari Ngugi

Lover of life, lover of big boobs and certified celebrity squasher. Catch me if you can on facebook as Irari Ngugi