Shilole afunguka kuhusu sababu ya kuficha mahusiano yake na mchumba wake mpya

Shilole atakua mke wa mtu hivi karibuni – staa huyo wa Bongofleva tayari ameshamtambulisha mchumba wake kwa wazazi wake.

“Nimepata mchumba mwenyeji wa Arusha na tayari nimeshatambulishwa ukweni. Soon dada Mwajuma naenda kuvaa shela. Nataka ndoa yangu kila mtu ahudhurie, nijaze uwanja wa Taifa. Ndoa itafungwa juu ya ndege tutashukia uwanja wa Taifa,” Shilole alisema kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM.

download latest music    

Mrembo huyo pia alifunguka kuhusu sababu ya kuficha mahusiano yake na mchumba wake mpya. Shilole alisema anahofia kuyaweka mahusiano yake wazi kwasababu mahusiano yake ya awali yalivunjika kutokana na kuwekwa zaidi hadharani.

“Mahusiano yangu ya nyuma yalivunjika kwa sababu niliyaweka wazi kwa watu wa karibu. Kwa sasa, namficha mume wangu mtarajiwa,”  Alisema Shilole.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere