Show kubwa ya Rayvanny na Akothee yaandaliwa Ujerumani

Ndoa baina ya wasanii kutoka Kenya na Tanzania yazidi kukita mizizi. Ushirikiano kati ya wasanii wa Kenya na haswa wasanii wa Wasafi unazidi kuongezeka kila uchao.

Hivi juzi Rayvanny alifanya collabo na msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya anayeitwa Bahati. Msanii Willy Paul pia alitia sahihi na Wasafi kuuza wimbo wake kwenye tovuti la Wafasi.com.

download latest music    

Sasa Rayvanny na Akothee watatumbuiza mashabiki katika jiji la Frankfurt nchini Ujerumani. Wawili hao wataperform katika Black Light Centre Costpark Aprili 15.

Akothee ashawahi kufanya collabo na Diamond, wawili hao walitoa wimbo unaoitwa ‘Sweet Love’ Januari mwaka uliyopita.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere