Staa wa bongo movie Salma Jabu maarufu Nisha Bebee asema ukweli kuhusu mimba aliyopata baada ya kubakwa

Akiongea katika AyoTV, Salma Jabu alisema kuwa hana mimba. Staa huyo alieleza kuwa watu hawajui kutafautisha Salma na Nisha.

“Kwanza kabisa kila kitu kinatokea kwasababu. Kwa wale ambao wametokea kuwa wananichunguza au kunifwatilia tangu nlianza safari ya sanaa mbaka hapa nimefika, Nisha sio mtu wa kumwakilisha Salma katika media. Unapomzungumzia Nisha humzungumzi Salma. Ninacho maanisha ni kwamba Yule ambaye ana mimba sio Salma, ni Nisha. Ndo maana nkasema kila kitu kinatokea kwa sababu Nisha huwa hapendi kumrepresent Salma katika media,” Salma alisema.

download latest music    

Alifafanua kuwa alimvaa mtu anayeitwa Mariana ile kumpresent katika jamii kama mtu aliyepata mimba baada ya kubakwa.

“Ahhh! Sina mimba, mimi ni balozi wa watoto waishio katika mazingira hatarishi. Kwa hio kama balozi nliamua nifanye uchunguzi. Katika uchunguzi huo nliamua kutengeneza filamu ambayo ndo chanzo cha watoto asilimia sabini na tano wanaoishi katika mazingira hatarishi. Kuna wazazi ambao walibakwa wakaja wakajifungua watoto wakawatupa wakaja wakaokotwa, kuna wazazi ambao …mambo mengi amboya mwanamke amekua akiyapita kwa maisha yake yakasababisha kuja kuzaliwa wale watoto wa mitaani. Kama nlivyokuambia apo awali napenda kufanya uchunguzi katika filamu zangu, nliamua kumvaa mtu anaitwa Mariana na nikampresent katika jamii alafu nkisema story yake kwa ufupi katika mtendao wa kijamii, nkaandika story ya ule mtu lakini the way ambavyo watu walipokea, ilinipa shauku ya kutaka kubeba ule uhusika zaidi na kuja kujua maumivu ambayo ntakuja kuyapata au Yule mtu ambaye amepitia kubakwa vitu kam hivyo ambavyo anaweza akazipata,”

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere