Tabia Za Maisha Zinavyoweza Kuathiri Afya Ya Ubongo

Kuna baadhi ya vitu tumekuwa tunavifanya lakini bila kujua kwa kasi gani vinaweza kuathiri afya ya miili yetu au baadhi ya viungo vya miili yetu, inaweza isiwe kwa mara moja lakini kadri tunavyozidi kufanya  madhara yake tunaweza kuja kuyapata baadae.Hizi ni baadhi ya tabia za kimazoea ambazo zinaathiri  afya ya akili.

1.Uvutaji wa Sigara

download latest music    

Kwa zamani kidogo ilizoeleka uvutaji wa sigara ni kwa watu wazima lakini sasa hivi hadi vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji wa sigara,tendo  hili ufanya kugandamana kwa ubongo na kuleta ugonjwa unaojulikana kama Alzheimer.Madaktari wanasema kuwa chembe za moshi zinazohathiri mapafu,huaribu mishipa midogomidogo ya kumbukumbu pia.Hivyo kumfanya mtu kuwa na uwezo mdogo wa kukumbuka.

2.Kuwa na Hasira Kwa Muda Mwingi.

kitendo cha kuwa na hasira hufanya mishipa ya ubongo kuzidiwa nguvu na  hivyo kupunguza uwezo wa akili kufanya kazi vile ipasavyo.

3.Kufanya Kazi kwa Muda Mrefu

Imekuwa ni kama desturi kujilazimisha kufanya kazi tukitaka kuimaliza bila kujali ni muda gani umefanya kazi na unahitaji kupumzika.hii inatokea kwa watu wengi sana hasa wale wanaofanya kazi za ofisini zinazohitaji muda mwingi wa kutumia akili.tabia hii inachoshwa ubongo na kuufanya kupoteza ufanisi wa kazi zake.

4.kukosa kulala vya kutosha.

kulala ufanya ubongo kupumzika na kujirutubisha tena vya kutosha.endapo mtu atakosa muda mrefu wa kulala na kupumzika ufanya  seli za ubongo kufa, hivyo hii uharibu ubongo zaidi.

5.Kuvuta Hewa Chafu kwa Muda Mwingi

Hii uchangiwa na mazingira yetu ya kazi au maeneo tuyayoishi,ubongo utumia oksijeni kwa kiasi kikubwa ili kuweza kufanya kazi, lakini endapo tutakuwa katika mazingira yanayosababisha kuvuta hewa chafu inapunguza kiasi cha oksijeni katika ubongo hivyo kuathiri ubongo wa kiasi kikubwa sana.

Shida ni kwamba, hali zetu za maisha au hali za mazoea na kutokujali ndipo kunakosabaisha madhara na magonjwa haya ambayo ni vigumu kuyagundua kwa urahisi.Hivyo basi swala la afya linaitaji kuangaliwa sana hasa tuapoamua pia kuchagua mitindo ya maisha tuanayoishi.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.