‘Sasa Mimi Ni Mtu Mpya’ Amekiri Dudubaya Baada ya Kudai Kamrudia Mungu

Msanii mkongwe wa Bongo fleva maarufu kama Dudu Baya amefunguka na kuielezea hadhara katika barua ya wazi kwamba ameamua kumrudia Mungu.

Dudu Baya alishika sana vichwa vya habari kwa mwaka uliopita wa mwaka 2017 kuanzia bifu lake na msanii mwenzake Mr. Nice kunyemelea kutaka kirudi tena na wawili hao kusikika wakianza kurushiana tena maneno upya mpaka ishu ya Young Dee kuiba wimbo wake.

Lakini Dudu Baya amesema anauanza mwaka huu wa 2018 upya kabisa huku akidai kwamba ameamua kumrudia Mungu wake na kuachana kufanya matendo ambayo hayampendezi.

Dudu Baya amefunguka hayo kwenye mahojiano na Bongo 5 ambapo amedai kuwa hii ni barua ya wazi na shukrani yake kwa kuuona mwaka 2018:

Eeh Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na nchi na mimi mwanadamu na vitu vyote vilivyomo asante baba mwezi wa tano mwaka 2017 nilimchoka shetani wa pombe si rahisi kumuacha kama mtu hajakushirikisha wewe mwenyezi Mungu huwezi kumuokoa asiye tayari kuokolewa 2017 asante baba umeniokoa mwaka 2018 nauanza nikiwa mamba Dudubaya, oil chafu konkii master new person new life pombe alininyima muda wa ibada pombe alininyima muda wakutimiza majukumu yangu pombe alininyima muda wa kuzuia hasira zangu sasa mimi ni mtu mpya”.