Baraka The Prince afichua sababu ya kukataa pendekezo kutoka kwa director aliyemtoa msanii Steven Kanumba

Steven Charles Kanumba alikuwa msanii aliyetajika kwa mapana na marefu kwa filamu za Bongo flava. Kanumba aliaga dunia 2012 na mbaka wa leo hakuna msanii mwingine amevuma kumliko.

Steven Charles Kanumba

Kanumbo alitolewa na director mkongwe katika tasnia ya filamu maarufu kwa jina la Mtitu. Director huyo alimtaka Baraka The Prince ajiunge na filamu za Bongo fleva lakini mwimbaji huyo alikataa pendekezo hilo.

Akizungumza na Eatv, Baraka The Prince alieleza kuwa alikataa pendekezo hilo kwa sababu bado alikua anajenga jina katika sanaa muziki.

“Nilishafuatwa kabisa na yule ‘director’ Mtitu aliyemtoa Kanumba alikuwa anataka tufanye ‘series’ mimi niwe ‘starling’ na Irene Uwoya lakini kwa kipindi kile sikuwa ‘ready’ kuingia kwenye mambo ya ‘movie’  lakini bado sijawa ready kwasasa hivi kwasababu bado najenga Brandy yangu,”alisema Baraka The Prince.

Baraka The Prince