Mwakyembe Amkumbuka Kanumba, Ataka Familia Yake Inufaike.

Waziri wa habari Tamaduni na michezo Mh Harison Mwakyembe ameanza michakato ya kuwasaidia wasanii katika kufanya mikataba iliyokamilika ili kupunguza wimbi la wasanii wanaosaini mikataba isiyokuwa na tija kwa wasanii hao.

Wazir Mwakyembe ambae alianzisha sakata hili hivi karibuni baada ya Mzee Majuto ambae ni msanii na mkongwe katika tasnia ya maigizo kukosa pesa kwa ajili ya matibabu ilhali alishawahi kufanuya kazi za sanaa na matangazo kwa muda mrefu ambayo inawezekana yangemnufaisha sana na hata kupata pesa za matibabu.

Mh mwakyembe amesema kuwa atahakikisha hata wasanii marehemu watasaidia kupata haki zao ili ziweze kunufaisha familia zao.

tukimaliza na mzee majuto , tunaanza na marehemu kanumba  na msanii yoyote anaeona amesaini mkataba wa kijinga kijinga aje tuona tunamsaidiaje.leo hii mzee majuto yuko hospitali na amekosa hata laki tano kwa ajili ya matibabu , kwaio nimtumie mimi sio, na mnaelea sasa hivi maisha siyo….

zoezi limeshaanza na kama mnavyojua kuwa linaitaji weledi na pia utaratibu mzuri na umakini mkubwa hivyo tumeakiri kamati ya wanasheria watano  na wameshaanza kuchambua mikataba mbalimbali ya wasanii.

lakini kwa sababu swala lenyewe linabidi liende haraka haraka , basi tutaongeza baadhi ya wanasheria  wanne ili wafike tisa

 

Baraka The Prince afichua sababu ya kukataa pendekezo kutoka kwa director aliyemtoa msanii Steven Kanumba

Steven Charles Kanumba alikuwa msanii aliyetajika kwa mapana na marefu kwa filamu za Bongo flava. Kanumba aliaga dunia 2012 na mbaka wa leo hakuna msanii mwingine amevuma kumliko.

Steven Charles Kanumba

Kanumbo alitolewa na director mkongwe katika tasnia ya filamu maarufu kwa jina la Mtitu. Director huyo alimtaka Baraka The Prince ajiunge na filamu za Bongo fleva lakini mwimbaji huyo alikataa pendekezo hilo.

Akizungumza na Eatv, Baraka The Prince alieleza kuwa alikataa pendekezo hilo kwa sababu bado alikua anajenga jina katika sanaa muziki.

“Nilishafuatwa kabisa na yule ‘director’ Mtitu aliyemtoa Kanumba alikuwa anataka tufanye ‘series’ mimi niwe ‘starling’ na Irene Uwoya lakini kwa kipindi kile sikuwa ‘ready’ kuingia kwenye mambo ya ‘movie’  lakini bado sijawa ready kwasasa hivi kwasababu bado najenga Brandy yangu,”alisema Baraka The Prince.

Baraka The Prince