Anerlisa Aanika Siri Yake Iliyompunguza Kilo 49

Mpenzi wa Msanii wa Bongo fleva Ben Pol, Anerlisa Mugai ambaye anatokea nchini Kenya Amefunguka na kuweka wazi Siri Yake iliyomsaidia kupungua kilo 49.

Anerlisa aliibua mjadala mzito nchini kwao Kenya baada ya kupotea katika Mitandao ya kijamii kwa mieiz Tisa alipokuwa mnene na kuibuka akiwa mwembaba na aliyepunguza zaidi ya kilo 49.

Katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari, Anerlisa mwenye ukwasi mkubwa akitajwa kumiliki kiwanda cha maji ya kunywa alifunguka na kuianika ratiba yake iliyompa mafanikio makubwa:

Katika miezi miwili ya mwanzo nilipotaka kupungua nilikuwa ninafanya mazoezi mazito kwa muda wa saa moja kila siku. Mazoezi haya yalijumuisha kutembea na mazoezi ya mwili ya kujikunja (yoga).

“Miezi minne iliyofuata nilifanya mafunzo ya matumizi ya viungo kwa msaada wa mwanajeshi mstaafu. Hapa ndipo nilipopoteza uzito mkubwa wa kilo 30 kwa miezi hiyo minne kisha kilo 17 miezi mingine iliyofuata.

“Niliendelea na mafunzo hayo ambapo huwa ninatumia saa moja kila siku kwa ajili ya mazoezi”.

Mimi mwenyewe niliamua kusitisha kabisa matumizi ya sukari. Situmii vitu vya sukari kabisa. Niliamua kuwa ninapikia mafuta ya olive ambayo hayanenepeshi tofauti na mafuta mengine. Napendelea vyakula vya kuchemsha au kukausha kama nyama. Huwa ninapima kiwango cha ‘kabohaidreti’ kwa kijiko cha chai. Pia ninakunywa maji mengi hadi lita tano kwa siku. Napendelea vyakula vya protini kama maharage kwani ukila kidogo tu hushibisha kwa muda mrefu bila madhara ya kusababisha unene.

“Nakula sana mboga aina ya sukuma wiki na spinachi kwa wingi kwa ajili ya kupata vitamini”.

 

Msanii Wyse Amtetea Ben Pol Dhidi Ya Tetesi Za Kuwa ‘Kibenteni’

Msanii wa muziki wa Bongo fleva maarufu kama Wyse ambaye Hivi sasa anatamba na single yake ya ‘Chota’ Ameibuka na kumkingia kifua msanii mwenzake Ben Pol.

Ben Pol amekuwa akitengeneza headlines na Mpenzi Wake Mpya Anerlisa ambapo mrembo huyo anatajwa kutokea kwenye Familia yenye mkwanja mrefu kiasi ya kwamba inasemekana Hivi sasa anamlea Ben Pol.

Msanii Wyse ameibuka na kukataa kabisa taarifa na hizo na kusema wazi kuw Ben Pol sio kibenteni na wala hayupo na mwanamke Yule kwa ajili ya pesa kama wengi wanavyodhani bali ni mapenzi ya dhati kwani tayari Ben Pol ana pesa zake binafsi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari Wyse amefunguka haya kuhusu mahusiano ya Ben Pol na Mpenzi Wake Anerlisa:

Ben Pol pia ana mkwanja mrefu pia yaani kwa kifupi ni kwamba pale hakuna mtu ambaye anamlea mwenzake, ni watu ambao wameridhiana”.

 

Mahaba Mazito, Anerlisa Ajibu Mapigo Kwa Ben Pol

Mwanadada Anerlisa Muigai ambaye yuko kwenye mahusiano na staa wa Bongo fleva Bernard Paul ‘Ben Pol’ ameonekana kujibu mapigo kwa Mpenzi Wake Baada ya kumtumia ujumbe wa kimahaba.

Siku ya jana Anerlisa alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa na Mpenzi Wake Ben Pol alimtumia ujumbe mzito Man kumuambia ni Jinsi gani anampenda na uzito alionao kwake.

Lakini inaonekana wapendanao hao wapo kwenye mahaba mazito kwani Anerlisa ameamua kumjibu Mpenzi wake kwa ujumbe mwingine ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Anerlisa ameandika maneno haya:

Asante Ben Pol kwa kuwa mtu nzuri na kuniletea Furaha kwenye maisha sitaki kusema meng lakini naomba niseme kuwa unanishangaza kila siku  Mwenyezi Mungu akubariki kuliko matarajio yako na akupe maisha marefu”.

https://www.instagram.com/p/Bscla8dg7XC/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1uz0ojt04n8l2

“Maneno Hayawezi Kueleza ni Jinsi Gani Nakupenda”- Ben Pol

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol ameibuka na kumtumia ujumbe mzito wa kimahaba Mpenzi wake Anerlisa.

Siku ya jana Anerlisa alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ameweka wazi kuwa anafikisha miaka 31 na Ben Pol alimtumia ujumbe mzito ambao ulikuwa na maneno matamu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ben Pol ameweka picha moja na video mbili ambazo zilikuwa zimeambatana na maneno yanayosomeka:

Happy Birthday My Love @anerlisa .. Words Cannot Explain How Much I Love You (Maneno hayawezi kueleza jinsi gani navyokupenda) ?, Nakutakia Maisha Marefu Na Furaha. May All Your Dreams Come True..(nakuombea ndoto zako zitimie) #MyQueen ??❤???”.

Mc Pilipili Amtaka Ben Pol Amuoe Mpenzi Wake Mpya

Mshehereshaji maarufu Emmanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili ameibuka na kumpa ushauri staa wa Bongo fleva Ben Pol wa kumtaka amuoe Mpenzi Wake Mpya.

Wiki chache zilizopita Ben Pol alianika mapenzi yake hadharani na binti wa Kikenya anayeitwa Anerlisa Mugai ambaye anatajwa kuwa mtoto wa kigogo na pia binti anayeogelea kwenye pesa.

 

Mc Pilipili ameibuka na kutia neno kwenye mahusiano ya Ben Pol na Anerlisa ambapo  amesema watu wa kabila lake siku zote huwa wanapenda kweli kweli, hivyo akamtaka Ben Pol kuchukua maamuzi ya kuoa.

Wagogo tukipenda hua tunapotelea kabisa Ben Pol nakuelewa kaka yangu huu mwaka wetu kama tulivyoongea kaka”.

Mc Pilipili amekuwa kwenye headlines kwa siku mbili hizi Baada ya video yake alipokuwa anamvisha pete Mpenzi Wake na kuangua kilio  kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii.

Ben Pol Azama Ndani Ya Penzi Zito na Mtoto Wa Bilionea Wa Kenya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amedaiwa kuzama ndani ya Penzi zito Mtoto wa Bilionea kutoka nchini Kenya anayeitwa Tabitha Karanja.

Binti ambaye anatajwa kuwa kwenye mahusiano na Ben Pol  anaitwa Anerlisa Mugai mwenye umri wa miaka 30 ambaye pia mfanyabiashara.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo, Sio Mbaya ameonekana kuwa karibu zaidi ya Anerlisa ambaye ni bosi wa kampuni ya kutengeneza maji ya chupa iitwayo, NERO company ambayo inazalisha maji ya Executive.

Kwa sasa wawili hao kwa pamoja wamekuwa wakisafiri sehemu mbalimbali za dunia. Hivi karibuni muimbaji huyo alionekana akiwa amepanda first class emirates ambayo inakadiriwa ni zaidi ya tsh milioni 40 kwa tiketi moja.