Ben Pol amsifu mwanae wa kiume baada ya kutimiza mwaka mmoja mwezi huu

Ben Pol amezipost picha mpya akiwa na mwanae wa kiume, Mali aliyetimiza mwaka mmoja mwezi huu na kulingana na maoni ya mashabiki wake wa Instagram mtoto huyu anapendeza sana kama babake.

Ben Pol na mwanae, Mali
Ben Pol na mwanae, Mali

Picha hizi zimekuwa zikiwakosesha wengi usingizi kwa kuwa wengi bado hawajatosheka kumtamani mtoto huyu. Ata hivyo Ben Pol ameweza kufunguka kumhusu na huku akizungumza na Bongo 5 alisema kuwa mwanae ameonyesha kuwa anavipaji vingi kama anapenda kucheza na mpira na pia anapenda sana kuimba na mamake nyimbo za kitoto.

Ukimpa mpira anapenda kucheza sana kwa mikono, anapenda kudundadunda sana mpira.Lakini vile vile pia mama yake anaimbaga naye mara nyingi sana, nyimbo za kitoto. Mama yake akiwa anaimba anamfuatisha sijui sauti ya pili, sijui anaimba sauti ya ngapi. Kwahiyo anaonekana anapenda kuimba, anapenda mpira, kwahiyo sijui itakuwaje, sijui atakuwa mcheza mpira sijui atakuwa muimbaji, lakini all in all nashukuru Mungu anakua vizuri.

Ben Pol na mwanae
Ben Pol na mwanae

Ben Pol aliongeza kwa kusema kuwa bado wanaendelea kumuangalia ili waweze kujua kipaji chake lakini kwa hivi sasa yeye na mamake mtoto hawana haraka.

Ila kiukweli kwenye kipaji hapo bado tunaendelea kuangalia sababu kiukweli anatuchanganya, atakuwa Shaquille O’Neal au atakuwa R.Kelly, hapo ndio au atakuwa Ben Pol au atakuwa Hasheem Thabeet.