Calisah Kuja Na Project Ya Kugawa Mimba Kwa Kinadada

Moja ya models wanaofanya vizuri Tanzania calisah ambae hivi karibuni mashabiki walikuwa wakimtukana baada ya kupiga picha akiwa anatangaza bidhaa za viati vya kike .Imekuwa ni tabia ya baadhi ya mashabiki kuwatuhumu sana models wa kiume na kuwahusisha na mapenzi ya jinsia moja kutokana na tabia zao kufanana na tabia za kike(tabia za ushoga).

Calisah amewajia juu wanaoendelea kumtukana katika mitandao, lakini ametoa mpya baada ya kusema kuwa anakuja na project mpya ya kutoa mimba kwa wakina dada ambao wapo mjini na wanatembea na wanaume wenye ela lakini wanashindwa kuzaa nao kwa sababu tu wanamuonekano mbaya,hivyo kwa kuwa yeye anamuonekano mzuri basi atajitolea kuwasaidia wadada wote wazuri mjini ambao wanataka kuzaa watoto wenye sura nzuri kama ya kwake.

“suala la kuzaa mimi mwenyewe nilikuwa na plan kwa sababu nilishatoka na wanawake wengi sema tulikuwa hatujakubaliana tu, na sikuwa tayari kuzaa kwa sababu bado nilikuwa kijana mdogo.Hawa wote nilikuwa nao tu kwa mambo mengine , lakini kama kuna mtu anataka tuzae,naweka tu dau langu ,tunapiga tu papapaaaa inatokea pair flani kali.Na ninajua mtoto wangu atakuwa na maisha mazuri maana hata kama babake ntafulia najua mamake yupo ana ela ataweza tu kumlea na atakuja kunisaidia”  alifunguka Calisah

Calisaha nasisitiza kuwa wapo wadada wengi sana mjini anaowajua wanatembea na wababu vikongwe kwa sababu tu ya ela, lakini sasa kwa sababu yeye ana sura nzuri, basi atawasaidia waweze kuzaa ilimradi tu waweke dau lake mezani yeye wala hana shida”tunawajua wasnii weng sana wazuri ambao wanaishi na wazee wanamapengo, macho yameingia ndani, lakini anayo ela, anajikuta  anazaa nae kisa ela tu tusijidarau wanaume kama mtu anaelaunaweza kumfanyia chochote iyo ni fursa.mimi ni kudume nanyoosha tu ilimradi aje tu na ela yake , kama wanawake wazuri wanatembea na watoto wazuri kwanini sisi wanaume tusifanye hivyo’  aliongezea Calisah

Hivi karibuni calisah alikaririwa akisema kuwa yuko tayari kuutumia mwili wake kufanya kitu chochote kile ambacho yeye anaona kitamuingizia ela katika maisha.

 

Calisah Afunguka Kuhusiana na Picha Zake Zilizovuma Mtandaoni (picha)

Mwanamitindo Calisah amefunguka kuhusiana picha zake zilizoenenea kwenye mitandao ya kijamii kuanzia weekend iliyopita.

Picha hizo zilizowekwa mitandaoni na Calisah mwenyewe ambazo zinamuonyesha akiwa amevaa viatu virefu vya kike, picha hizo zileta gumzo huku watu wengi walioshangazwa na pica hizo ni wanaume ambao hawakuelewa kwa nini model wa kiume avae viatu vya wanawake.

Hizi ni picha za Calisah zilizoleta gumzo mtandaoni;

.
.

Kwenye Mahojiano aliyoyafanya na Millard Ayo Calisah alifunguka yafuatayo;

“Tulipiga zile picha kwaajili  kufanya tangazo la TV la viatu Kama inavyonekana lakini kuna mtu akazichukua akataka kuzivujisha au apewe hela kwaiyo mi nikaziweka mwenyewe mtandaoni lakini watu wakitaka waelewe wasubiri tangazo litoke, anyway tangazo lenyewe Mimi ninakuwa naelezea viatu ninavyopenda demu wangu avae ndo nikawa namuonyesha nanikavivaa kwenye tangazo ndo picha zikapigwa”.

Calisah aliendelea kufunguka kuwa ameshangazwa na watu kumuita shoga wakati ile ni kazi tu na kudai yeye yuko sawa na ni kidume Kama kawaida na wala sio shoga Kama watu wengi walivyozusha.